Haji akabidhi ripoti ya uchunguzi wa KEMSA kwa Tume ya EACC

Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amerudisha ripoti ya uchunguzi wa Bodi ya KEMSA kwa Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi nchini EACC kwa ajili ya uchunguzi zaidi.

Haji pia amewaagiza waendesha mashtaka wakuu waliochaguliwa kuchunguza ripoti hiyo wafanye vikao vya pamoja na tume ya EACC ili kuharakisha uchunguzi huo.

Hii ni baada ya Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma kupata mapengo katika uchunguzi wa malipo yenye dosari ya shilingi bilioni 7.8 ya vifaa vya kupambana na COVID-19 yaliyofanywa na KEMSA.

Also Read
Gavana Kinyanjui asema hospitali za Nakuru zimejaa wagonjwa wa korona kutoka kaunti jirani

Kwenye taarifa yake Haji, amesema japo swala hilo linapewa kipau mbele, lazima kuwe na ushahidi wa kutosha kabla washukiwa wa ufujaji wa pesa hizo washtakiwe.

Baada ya uchunguzi hapo awali, Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma ilipendekeza kushtakiwa kwa maafisa wakuu sita kutoka Bodi ya KEMSA wanaosemekana kuhusika katika mchakato wa uagizaji wa vifaa vya COVID-19 uliopelekea bodi hiyo kufanya malipo ya Shilingi bilioni 7.8 kwa kampuni mbali mbali.

Also Read
Haji aidhinisha kushtakiwa kwa wahusika wa sakata ya zabuni za usambazaji umeme

Hata hivyo, kulikuwa na uchunguzi zaidi uliokuwa ukifanywa na Tume ya EACC kuhusu mchakato wa uagizaji wa vifaa hivyo na wale walionufaika na ulipaji wa mabilioni hayo.

Afisi ya Haji imekiri kuwa baada ya uchunguzi zaidi uliofanywa na timu ya waendesha mashtaka huru, iligundulika kuwa uchunguzi huo unafaa kufanywa kwa kina zaidi na kuwa kuna mashahidi kadhaa, taasisi na maelfu ya stakabadhi ambazo hazijafanyiwa uchunguzi vizuri.

Also Read
KEMSA yasambaza barakoa kwa wanafunzi wasiojimudu nchini

Timu hiyo ilipata maswala muhimu ambayo yanapaswa kuangaziwa kikamilifu kabla uamuzi wa mwisho kuhusu mashtaka kufanywa.

Aidha, Haji amesema wachunguzi wake watazingatia ripoti maalumu yake Mratibu wa Fedha za Serikali Nancy Gathungu kuhusu matumizi ya fedha za COVID-19 iliyowasilishwa kwa kamati ya pamoja ya Seneti kuhusu afya na maswala ya COVID-19.

  

Latest posts

Ruto: Mawakala wa kisiasa waliboronga uhusiano wangu na Rais Kenyatta

Tom Mathinji

COTU yazusha kuhusu nyongeza ya bei za mafuta nchini

Tom Mathinji

John Munyes na Charles keter kufika mbele ya Senate kuhusu ongezeko la bei ya mafuta

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi