Haji akariri kwamba wahusika wa kashfa ya KEMSA watachukuliwa hatua

Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji amewahakikishia Wakenya kwamba uchunguzi kuhusu kashfa ya KEMSA ungali unaendelea na kwamba waliohusika watashitakiwa.

Haji wakati uo huo amekanusha madai kwamba tume ya maadili na kupambana na ufisadi haitekelezi wajibu wake dhidi ya ufisadi ipasavyo.

Also Read
kaunti ya Nakuru yatenga shilingi bilioni 1.1 kugharamia miradi ya maji

Amesema kundi la wataalamu lililobuniwa linakusanya ushahidi kuhusiana na kashfa hiyo.

Haji ameongeza kuwa kuna udhifu kwenye harakati za  kutafuta ukweli kuhusu kashfa hiyo.

Haya yanajiri baada ya malalamishi kutoka kwa viongozi na Wakenya kuhusu kucheleweshwa kwa uchunguzi na kutochukuliwa hatua kwa watu waliotajwa kwenye kashfa hiyo.

Also Read
Shule moja Baringo yaelekea mahakamani kushinikiza kufukuliwa kwa mwili uliozikwa mbele ya darasa

Halmashauri ya Usambazaji vifaa vya matibabu nchini KEMSA inakashifiwa kwa kutoa kandarasi za usambazaji wa vifaa hivyo kwa kampuni mbali mbali bila kufuata sheria za kandarasi ipasavyo.

Inadaiwa kwamba kutokana na hayo, Kenya ilipoteza mamilioni ya fedha kiufisadi, fedha zilizonuiwa kusaidia nchi hii katika juhudi za kukabiliana na janga la COVID-19.

Also Read
Wakazi wa Kisii wasusia hospitali, wajitafutia dawa ya Korona

Rais Uhuru Kenyatta alikuwa ameagiza uchunguzi ufanywe na wahusika kuchukuliwa hatua za kisheria katika muda wa siku 21, muda ambao uliisha.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi