Haji Manara Aridhia Ombi la Balozi wa Burundi

Haji Manara au ukipenda Bugatti ni msemaji wa klabu ya soka ya Yanga nchini Tanzania na ametangaza kwamba amekubali ombi la balozi wa Burundi nchini Tanzania Bwana Gervas Abayeho. Ombi la balozi huyo kwa Manara ni kwamba asaidie kutangaza mechi ijayo kati ya timu ya taifa ya Burundi almaarufu The Swallows na ile ya Cameroon au ukipenda The Indomitable Lions.

Also Read
Trump aonywa dhidi ya kutumbukia mtegoni kuhusu madai ya vita kati ya Marekani na Israeli

Mechi hiyo itachezwa tarehe tisa mwezi Juni mwaka huu, katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam uwanja ambao unachukuliwa kama wa nyumbani wa timu ya Burundi baada ya uwanja wao mjini Bujumbura kupigwa marufuku kwa matumizi.

Also Read
Pompeo: Afisa wa ngazi ya juu Urusi aliamuru Navalny apewe sumu

“Balozi aliniambia jinsi shirikisho la soka nchini Burundi na mashabiki wa Soka wanaridhishwa na kazi yangu ya hapa nyumbani na kuomba nisaidie kuhamasisha ili watanzania na wazaliwa wa Burundi wanaoishi hapa nchini hususan Dar es salaam, waje Kwa wingi siku hiyo ya kuwania kufuzu kwa mashindano ya kombe la mataifa bingwa barani Africa Afcon mwaka 2023 huko Ivory Coast.” aliandika Manara.

Also Read
Marekani kuwapima watu milioni 500 ugonjwa wa Covid-19 bila malipo

Manara ambaye awali alihudumu kwenye timu ya Simba SC, anasema amekubali ombi hilo kwa sababu ya ujirani mwema na moyo wa jumuia ya Afrika Mashariki na kwamba ameruhusiwa kutangaza mechi hiyo na Yanga SC ambayo anaifanyia kazi.

  

Latest posts

Waakilishi wa Kenya ,Prisons na KCB wasajili ushindi wa pili mashindano Afrika kwa Voliboli ya vidosho

Dismas Otuke

Kenya na Zimbabwe zafungiwa nje ya mechi za kufuzu kombe la AFCON mwaka ujao nchini Ivory Coast

Dismas Otuke

Watu 30 watekwa nyara nchini Nigeria

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi