Hali ya tahadhari yawekwa katika Mahakama ya Thika

Maafisa wa polisi mjini Thika wako tahadhari kufuatia habari za uwezekano wa kutokea kwa shambulizi la kigaidi linalolenga mahakama ya Thika.

Onyo hilo lilisababisha vikao va mahakama kucheleweshwa kwa saa kadhaa jana huku usalama ikiimarishwa nje ya mahakama hiyo na katika makao ya naibu wa kamishnna wa kaunti.

Also Read
Chuo cha MKU chatambuliwa katika kupunguza ukosefu wa usawa

Kulikuwa na ukaguzi mkali siku ya Jumatano kwa waliokuwa wakiingia mahakamani humo pamoja na afisi ya naibu wa kamishna wa kaunti wa eneo hilo.

Also Read
Serikali yatetea hatua ya kufunga barabara ya Thika jana usiku

Naibu wa kamishna wa kaunti anayesimamia eneo la Thika magharibi Mbogo Mathioya, alisema habari za kijasusi kuhusu uwezekano wa shambulizi kutokea zilitolewa siku ya Jumatano, hali iliyowafanya kuchukua hatua za haraka ili kuepusha hatari yoyote kutokea.

  

Latest posts

Ngirici aondoa kesi mahakamani kupinga ushindi wa Gavana Waiguru

Tom Mathinji

Rais Museveni awaomba Wakenya msamaha

Tom Mathinji

Joyciline Jepkosgei apandishwa cheo hadi Sergeant baada ya ufanisi wa London Marathon

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi