Halima Kopwe Aibuka Mshindi wa Miss Tanzania Mwaka 2022

Halima Ahmad Kopwe binti wa umri wa miaka 23 ndiye mshikilizi wa taji ya mlimbwende wa taifa nchini Tanzania almaarufu Miss Tanzania mwaka 2022. Bi. Kopwe alivishwa taji usiku wa tarehe 20 mwezi Mei mwaka 2022 katika fainali za kinyang’anyiro hicho zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam nchini Tanzania. Alinyakua zawadi ya gari aina ya Mercedes Benz na pesa taslimu shilingi milioni 10 pesa za Tanzania.

Also Read
Emmanuel Ehumadu ashutumiwa kwa kukusanya pesa za mazishi ya Asuzu

Akizungumza na wanahabari baada ya kutawazwa mshindi, Halima Kopwe alitoa shukrani za dhati kwa waandalizi wa shindano hilo. Kwa washindani wake aliwasihi wasife moyo waendelee kujaribu tena na tena huku akisema yeye alishiriki kwa mara ya kwanza mwaka 2018 ambapo hakushinda lakini akajifunza mengi na sasa ameibuka mshindi.

Alipoulizwa jinsi anapanga kutumia pesa alizoshinda, Halima alisema ataziwekeza katika kujiboresha kama mpeperushaji wa bendera ya taifa la Tanzania katika shindano la ulimbwende ulimwenguni yaani Miss World. “Nataka nijiandae vyema ili nikifika pale nisiwe mshiriki bali niwe mshindani.” ndiyo maneno ya Halima Kopwe.

Also Read
Kobe Bryant kutuzwa

Shindano hilo lilianza na washindani 20 mchujo ukafanyika dadi jana ambapo walisalia watano bora. Kati ya watano bora kulitolewa taji mbali mbali kama vile Miss Talent, Miss Personality na Miss Popularity. Hii ndio orodha ya wote walioshiriki shindano hilo;

Also Read
Masharti ya Simba!

1. Agnes Satura
2. Amida Twaha
3. Angel Alfred Mtatiro
4. Angel Boniphace
5. Aqram Issmail Ramadhan
6. Basalyner Omary
7. Beatrice Alex Akyoo
8. Emmanuela Silayo
9. Glory Pontianus
10.Halima Ahmad Kopwe
11.Happyness Mrosso
12.Jenipha Temba
13.Jenipher seif Mohammad
14.Nasra Swalehe
15.Nazimizye adam Mdolo
16.Otaigo Mwema
17.Ruth Anthony Ngonja
18.Stella Joseph
19.Subilaga Ambangile Biligiti
20.Warda Robert

  

Latest posts

Msanii Kajala Masanja amsamehe Harmonize

Tom Mathinji

Tarrus Riley awasili nchini kwa tamasha la Koroga Festival

Tom Mathinji

Diamond Ajisifia Kuwa Mwanamuziki Bora Tanzania

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi