Hamisa Mobeto akerwa na maneno ya Baba Levo.

Huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya wanawake, Hamisa Mobeto ambaye ni mjasiriamali na mama wa watoto wawili ana machungu moyoni.

Hii ni baada yake kurushiwa maneno mazito na msanii ambaye pia ni mtangazaji wa Wasafi Fm Baba Levo. Baba Levo aliachia video inayomwonyesha akisema kwamba ikiwa Hamisa atapata mimba ya Fred Vunja Bei ambaye anadhaniwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi naye, watazaa mwehu au mbwa.

Kupitia Instagram stories, Hamisa amemjibu Baba Levo akisema “@officialbabalevo kusema kweli umenikosea sana. Sijui nimekukosea wapi lakini sioni kama ni sawa wewe kuniingiza kwenye drama ambazo sifahamu wala hazinihusu.”

Anaendelea pia kumwambia kwamba sio sawa kwa mwanaume ambaye amezaliwa na mwanamke kusemea mwingine kwamba atazaa mbwa hata kama atazaa na mwanaume gani, ilhali yeye mwenyewe maajuzi amefichua kwamba mke wake ana ujauzito na yuko karibu kujifungua.

Anasema pia kwamba hadhanii kwamba Baba Levo angefurahia kusikia dadake, mamake au mke wake akiambiwa maneno kama hayo na kusisitiza kwamba amemkosea sana.

Hamisa Mobeto ana watoto wawili, wa kwanza wa kike ambaye babake ni Francis Ciza maarufu kama Majizo ambaye amemuoa Elizabeth Michael maajuzi na wa pili wa kiume ambaye babake ni msanii wa muziki Diamond Platnumz.

Baba Levo na Fred Vunja Bei wanaonekana kuwa na ugomvi fulani kati yao isijulikane kisa na maana lakini amekuwa akimsuta Fred aache kujiona kama mungu na aache tabia kama za Uchebe.

Baba Levo amesema pia kwamba umefika muda wa kurudisha heshima yake aliyopokonywa kwa ajili ya umasikini wake. Msanii huyo amekuwa akirejelewa kama “Chawa” kwa tabia yake ya kusifia watu tajiri nchini Tanzania kwa nia ya kupata namna ya kujikimu kimaisha.

Mwezi Agosti mwaka jana, Baba Levo alisikika akimhimiza Fred kumwoa Hamisa Mobeto wakati wa hafla ya kufungua duka la “VunjaBei” huko Iringa kwani Hamisa ni mwanamke mzuri naye Fred ana pesa sasa haijulikani ugomvi wao umetokea wapi!

Inaonekana kwamba Baba Levo amekuwa akipata mavazi ya bure kutoka kwa mfanyibiashara huyo Fred Vunja Bei kwani huwa anamtangazia biashara yake, na sasa ameandika kwenye Instagram “Sivai Tena MANGUO yenu Ya Kuchanika Chanika. Mje Myachukue Tu. SIYATAKIIIII….!!!!”

  

Latest posts

Rayvanny Kumtambulisha Msanii wa Kwanza NLM

Marion Bosire

Dulla Makabila Ajiondolea Lawama

Marion Bosire

Mwigizaji Atoa Ilani Kwa Rais Museveni

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi