Harambee Stars kuondoka nchini Jumamosi kwa mchuano wa marudio dhidi ya Comoros

Timu ya taifa Harambee Stars itaondoka nchini Jumamosi kuelekea mjini Moroni kwa pambano la marudio dhidi ya wenyeji Comoros Jumapili hii.

Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mkondo wa kwanza uwanjani Kasarani,Stars watasafiri kwenda Comoros wakifahamu fika kuwa kushindwa na wenyeji kutazima ndoto yao ya kufuzu kwa dimba la AFCON mwaka 2022 nchini Cameroon huku pia ushindi kwa wenyeji ukiwaweka mguu moja ndani ya kipute hicho kwa mara ya kwanza.

Also Read
Ratiba ya usafiri kwa timu ya Kenya kwa Olimpiki yatolewa huku safari hizo zikianza wiki hii


Kenya ni ya pili kundini G kwa alama tatu kutoka na mikwangurano mitatu nyuma ya viongozi Comoros waliozoa pointi 5.
Kocha wa Kenya Jacob Mulee ana Imani kuwa watasajili ushindi katika pambano hilo .

Also Read
Uchaguzi wa kitaifa wa Fkf hatimaye waandaliwa


“Tunatarajia kupata ushindi katika mchuano wa Jumapili baada ya kucheza vizuri  Jumapili ,leo ingawa tulishindwa kutumia nafasi zetu vyema’’akasema Mulee

Also Read
FKF kubuni mbinu ya kuteua mwakilishi wa CAF Confed Cup

Kenya na Comoros kumenyana Jumapili kwa mara ya 5 mechi nne za awali zikiishia sare huku Kenya ikiwashinda Comoros katika mchuano mwingine.

Comoros wanawania kufuzu kwa fainali za Afcon kwa mara ya kwanza katika historia yao.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Sportpesa kurejesha ufadhili michezo nchini Kenya

Dismas Otuke

Vidosho wa Kenya wapigwa dafrao na Msumbiji mashindano ya kikapu Afrika

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi