Harambee Stars kuondoka nchini Jumanne kwenda Kampala kwa mechi dhidi ya Uganda

Timu ya taifa ya soka Harambee Stars inatarajiwa kuondoka nchini Jumanne kwenda Kampala Uganda , kwa mechi ya tano ya kundi E kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao.

Stars ilihamishia mazoezi yake hadi uga wa kitaifa wa Nyayo Jumatatu ambapo wachezaji wote wa humu nchink waliripoti kambini.

Uganda Cranes wakiwa mazoezini

Pambano hilo litachezwa katika Uwanja wa St Mary’s Kitende Alhamisi Novemba 11 alasiri ,wenyeji wakihitaji ushindi ili kusalia katika nafasi ya kufuzu kwa raundi ya tatu na ya mwisho.

Also Read
Ligi kuu ya Kenya KPL kuendelea Jumatano kwa mikwangurano minne
Also Read
Usimamizi mbaya wa FKF walaumiwa kwa kudorora kwa soka ya Kenya

Kenya ni ya tatu katika kundi hilo kwa alama 2 pekee baada ya mechi 4,Mali wakiongoza kwa pointi 10, wakifuatwa na Uganda kwa alama 8.

Katika pambano jingine Alhamisi Rwanda itawaalika Mali mjini Kigali.

Also Read
Onyango kucheza hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika kwa mara ya kwanza

Harambee Stars watacheza mechi hiyo bila pressure kwani tayari wamebanduliwa kufuzu kwa awamu ya mwisho.

Kenya watahitimisha ratiba dhidi ya Rwanda katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo tarehe 15 mwezi huu.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi