Harambee Stars kupimana nguvu tena na Taifa Stars Alhamisi saa tisa Nyayo Stadium

Timu ya Kenya Harambee Stars itashuka katiuka uwanja wa taifa wa Nyayo kwa mchuano wa pili wa kirafiki dhidi ya wageni Taifa Stars kutoka Tanzania Alhamisi Machi 18 .

Pambano hilo limehamishwa kutoka uga wa Kasarani ambao unafanyiwa ukarabati kwa mechi ya Kenya dhidi ya Misri Jumanne ijayo kufuzu kwa kombe la AFCON .

Also Read
Kenya kufungua dimba na Misri Jumatano mashindano ya Voliboli Afrika

Kulingana na FKF mchuano huo utang’oa nanga saa tisa alasiri na wala sio saa moja usiku ilivyopangwa awali.

Also Read
FKF yapata pigo baada ya mahakama kuzirejesha Mathare United na Zoo Fc ligini

Ni mechi ya pili ,mtawalia kwa Kenya na Tanzania kumenyana baada ya Harambee Stars kuwabwaga Tanzania magoli 2-1 katika mechi ya kwanza ya kirafiki Jumatatau iliyopita huku timu zote zikijitayarisha kwa mechi za kufuzu kombe la AFCON raundi ya 5 na ya 6 ya makundi tarehe 22 na 30 mwezi huu.

Also Read
Wanasiasa watakiwa kuweka maslahi ya wakenya mbele wakifanya kampeini

Kenya itawaalika Misri Jumanne ijayo huku Tanzania ikizuru Equitorial Guinea pia wiki ijayo kwa mechi za kufuzu kombe la AFCON.

  

Latest posts

Victor Wanyama astaafu soka ya kimataifa

Dismas Otuke

Nigeria watawazwa mabingwa wa kikapu Afrika baada ya kuibwaga Mali 70-59

Dismas Otuke

Shujaa yatwaa nafasi ya tatu Edmonton 7’s na kuzoa pointi 16

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi