Harambee Stars wataanzia wapi baada ya kubanduliwa kufuzu kombe la dunia na AFCON mwaka ujao?

Timu ya taifa ya soka ya Kenya Harambee Stars italizimika kurejea na kuanza kujiandaa kwa mechi za kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika AFCON mwaka 2023 na zile za kufuzu kwakombe la dunia mwaka 2026.

Hii ni baada ya kutimuliwa kwenye kinyang’anyiro cha kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao walipolazwa na Mali bao 1-0 katika kundi E Jumapili jioni ,wakisalia katika nafasi ya tatu kwa alama 2 kutokana na mechi 4 ,nyuma ya uganda iliyo na pointi 8 na Mali wanaongoza kwa alama 10.

Also Read
Mvutano kati ya FKF na timu 4 watishia kuathiri msimu mpya wa ligi kuu

Harambee Stars waliosalia na mechi mbili watasafiri kwenda Kampala kumenyana na Uganda tarehe 13 mwezi ujao , kabla ya kuhitimisha ratiba nyumbani siku tatu baadae kwa kuwaalika Rwanda.

Also Read
TSC kushirikiana na wadau wa elimu kuboresha masomo katika kiwango cha kaunti

Matokeo haya yanajiri miezi 6 baada ya Kenya pia kukosa kufuzu kwa kombe la bara Afrika mwaka ujao nchini Cameroon baada ya kumaliza katika nafasi ya tatu ,nyuma ya Misri na Comoross waliofuzu kwa kipute hicho.

Also Read
Kimanzi atawazwa kocha bora wa ligi kuu mwezi Januari

Licha ya kubadilisha wakufunzi mara kwa mara na kuchanganya wa nyumbani na wakigeni pamoja na kubadilisha wachezaji tatizo la Harambee Stars linaonekana kuwa mbali na suluhisho,huku ikionekana bayana kuwa huenda pana tatizo la uongozi wa soka ya Kenya.

  

Latest posts

Watu wanne zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Matabibu wataka Uchunguzi wa mipakani kuimarishwa kuzuia kuenea kwa Ebola

Tom Mathinji

Wabunge wa kaunti ya Kitui wataka baa la njaa kutangazwa janga la kitaifa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi