Harambee Stars yabweteka nyumbani na kwenda sare tasa na Uganda mechi ya kufuzu kombe la dunia

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeanza mechi za kundi E , kufuzu kwa kombe la dunia mwaka ujao kwa kutoka sare tasa dhidi ya Uganda Cranes katika mchuano uliopigwa Alhamisi alasiri katika uwanja wa kitaifa wa Nyayo.

Stars walianza vyema mchuano huo lakini kukosa mashambulizi kumewagharimu katika nusu ya tatu ya uwanja huku nahodha Michael Olunga akiwekwa mfukoni na mabeki wa Uganda kutokana na kukosa pasi za kuunganishwa kwake ili afunge.

Also Read
Rais Kenyatta awatunuku Shabana Fc Basi Jipya

Kuonyesha mkanganyiko katika uteuzi wa kikosi chake kocha Jacob Mulee alimtoa Lawrence Juma na kumjumuisha Eric Omondi anayepiga soka ya kulipwa nchini Uswidi katika kipindi cha kwanza lakini bado mchezo haukubadilika kipindi hicho kikiishia sare tasa.

Also Read
Harambee Stars hawana budi kuwashinda Mali Jumapili ili kusalia kwenye safari ya kwenda Qatar mwakani

Cranes walionekana kuwa wazuri sana wakijihami na kukata mashambulizi na pasi nyingi za Kenya zilizoelekezwa katika mlango wao.

 

Kwa jumla Kenya ilibuni mashambulizi 11 huku wakilenga mlango wa uganda mara moja pekee nao Cranes wakabuni nafasi 4 wakilenga mlango wa Kenya mara mbili.

Also Read
Ni kufa kupona kwa Vihiga Queens dhidi ya River Angels ya Nigeria Ijumaa

Uganda Cranes itarejea Kampala kuwaalika Mali ,Jumatatu katika uwanja wa Kitende nao Kenya wazuru Kigali kupambana na Amavubi ya Rwanda Jumapili tarehe tano Septemba kwa mechi za mzunguko wa pili.

Mali wanaongoza kundi hilo kwa pointi 3 baada ya kuwashinda Rwanda goli 1 -0 Jumatano usiku.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

KBC yafadhili timu ya magari itakayoshiriki mashindano ya Machakos Rallycross

DOtuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi