Harambee Stars yahitimisha mechi za kufuzu kombe la dunia kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Rwanda

Timu ya soka ya Kenya , Harambee Stars hatimaye ilisajili ushindi wa kwanza katika harakati za kufuzu kwa kombe la dunia , baada ya kuwacharaza Amavubi ya Rwanda mabao 2-1 katika uchanjaa wa kitaifa wa Nyayo Jumatatu Alasiri.

Also Read
Mabingwa wa ligi Thika Queens wanyofoa tuzo za KEFWA

Nahodha Michael Olunga alitumia vyema makosa ya mabeki wa Rwanda na kupachika bao la kwanza dakika ya tatu.

Dakika 10 baadae kiungo Richard Odada alitanua uongozi wa Kenya kwa bao la pili kupitia mkwaju wa penati baada ya Eric Ouma kuangushwa.

Also Read
Betsafe yazindua tuzo ya mchezaji bora kila mwezi kwa timu za AFC Leopards na Gor Mahia

Oliver Niyonzima aliifungia Rwanda bao moja kunako kipindi ,huku ngoma ikikatika kwa ushindi wa 2-1 , ukiwa ushindi wa kwanza kwa Harambee Stars katika mechi za kufuzu kombe la dunia.

Also Read
Casa Mbungo atua Bandarini kupiga ukufunzi kwa miaka miwili

Kenya ilimaliza ya tatu kundi E kwa jumla ya pointi 6 , nyuma ya Uganda iliyomaliza kwa alama 8 na viongozi Mali waliozoa pointi 14.

Rwanda ilizoa alama 1 pekee.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi