Harambee Stars yaimarika kwa nafasi 2 licha ya kipigo cha kitutu na Mali

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars imeimarika kwa nafasi mbili katika msimamo wa dunia wa FIFA wa mwezi jana uliotangazwa Alhamisi licha ya kucharazwa na Mali nyumbani na ugenini katika mechi mbili za kundi E, kufuzu kwa kombe la dunia mapema mwezi huu.

Also Read
Bingwa wa dunia Timothy Cheruiyot kuwika Kip Keino Classic Jumamosi

Kenya imepanda hadi nafasi ya 102 ulimwenguni kutokana nambari 104 iliyokuwa mwezi Agosti.

Also Read
Allan Muhanda ndiye mwenyekiti wa Fkf Kakamega

Ubelgiji ingali kuongoza msimamo wa dunia ikifuatwa na Brazil na mabingwa Ufaransa katika nafasi za pili na tatu mtawalia.

Nafasi ya nne ni Italia, Uingereza ya tano nao Argentina ,Uhispania na Ureno zimo katika nafasi za 6,7 na 8 katika usanjari huo.

Also Read
Ghana Black Satelites wafuzu fainali ya AfFCON U 20 wakiwinda kombe la 4

Mexico ni ya tisa kisha Denmark inahitimisha orodha ya 10 bora.

  

Latest posts

Amos Kipruto ashinda London Marathon huku Jepkosgei akimaliza wa pili kwa vipusa

Dismas Otuke

Malkia Strikers wabanduliwa mashindano ya dunia baada ya kipigo cha seti 3-1 na Puerto Rico

Dismas Otuke

Boubacar Kamara kutocheza kwa muda kutokana na Jeraha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi