Harmonize afungua mwezi Novemba na kibao kipya, “Ushamba”

Harmonize mjeshi au ukipenda Konde Boy mwanamuziki wa nchi ya Tanzania ana kibao kipya kwa jina “Ushamba”.

Mmiliki huyo wa kampuni ya wanamuziki kwa jina “Konde Music” alikizindua rasmi tarehe mosi mwezi Novemba mwaka huu usiku na wana Konde Gang na wengine ambao walihudhuria tamasha hilo kwa jina “Ushamba Night Party” walivaa kishamba.

Also Read
Dulla Makabila afunga ndoa

Maneno ya wimbo huo ni ya kukosoa watu kutokana na mambo ambayo wanafanya kila siku maishani na pia kuna sehemu ambapo anazungumzia washindandi ambao anasema sasa wanahofia yeye anawapita.

Baadhi ya maneno kwenye wimbo huo ni kama yafuatayo,

“Pesa ya kulipa gesti unayo, nyumbani familia inapiga miayo

Yanafurahisha ufanyayo? Huo ni Ushamba

Inaboa kudadadeki, dereva wa Uber hataki ku ovateki

Also Read
Panya Shujaa!

Eti kisa pesa iongezeke, Huo ni ushamba

Yupo Kitandani kajilegeza, nguo kaziweka kwenye meza

Nikishajipaka vya kuteleza, Eti bebi leo Simba wanacheza

Huo ni Ushamba …”

Mwanamuziki Nandy alihudhuria tamasha hilo la “Ushamba” ambapo alipanda jukwaani na kuimba na Harmonize ila yeye hakuvaa kishamba. Harmonize alimtania kidogo kwamba amenenepa kisa na maana anatunzwa vyema na mpenzi wake Bilnas.

Also Read
Issa Rae na Louis Diame wafunga ndoa

Pierre Liquid mchekeshaji ambaye anajulikana kwa maneno “Konki Liquid” naye alihudhuria tamasha hilo kati ya watu wengine maarufu nchini Tanzania.

Harmonize ambaye jina lake halisi ni Rajab Abdul Kahali anaonekana kuwa na mengi tu ambayo amewaandalia mashabiki wake mwaka 2020 unapokamilika.

  

Latest posts

Wasanii Wanaowakilisha Kenya AFRIMA

Marion Bosire

Akothee Apata Mgeni wa Heshima Kwenye Hafla Yake

Marion Bosire

KFCB Yazuia Usambazaji Wa Filamu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi