Harmonize Matatani Tena

Mwanamuziki wa Tanzania Rajab Abdul Kahali almaarufu Harmonize ameshtakiwa Mahakamani na mwanamuziki mwenzake Dully Sykes kwa madai ya kukiuka hakimiliki.

Dully anasema Harmonize alitumia maneno ya wimbo wake uitwao “Bongo Fleva” bila idhini na amekataa kumlipa.

Sykes anasema haki lazima itendeke Kwani Harmonize anaendelea kulipwa kutokana na wimbo ambao ameunda kwa kutumia maneno ya wimbo wake naye hapati chochote.

Also Read
Jacqueline Wolper amechumbiwa

Hakusema kiasi cha pesa ambacho anadai kutoka kwa mmiliki huyo wa kampuni ya kusimamia wanamuziki ya Konde Music Kwani kesi bado iko mahakamani.

Hii sio mara ya kwanza Harmonize analaumiwa kwa kutumia nyimbo za wengine na kukiuka hakimiliki.

Rosa Ree ambaye ni mwanamuziki wa Tanzania aliwahi pia kuibua madai sawia mwaka jana ambapo anasema Harmonize alitumia mdundo wa kibao chake kiitwacho “Kanyor Oleng”.

Also Read
Harmonize afungua mwezi Novemba na kibao kipya, "Ushamba"

Yapata wiki mbili zilizopita, Rosa Ree alifafanua kwamba walishamalizana na Harmonize Kwani alimlipa fidia kwa sababu ya kukiuka hakimiliki.

Mwanadada huyo alielezea kwamba alikuwa anapanga kufanya kazi na Harmonize ambapo alimwonjesha midundo yake lakini hata kabla waingie studio pamoja, Harmonize akaamua kutumia mdundo wake kutoa kibao chake binafsi.

Mr Nice, mmoja wa waanzilishi wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania naye aliwahi kusema kwamba Harmonize katumia mdundo wake bila idhini.

Also Read
Rita Ora ashtumiwa nchini Australia

Harmonize pia alitumia maneno ya mwanamuziki wa Kenya Stivo Simple Boy, “Inauma lakini inabidi tuzoee” bila idhini.

Kuna tetesi pia kwamba Harmonize amemrusha Nyota Ndogo maneno ya wimbo baada yake kuonyesha nia ya kushirikiana naye katika muziki.

  

Latest posts

Ogopa Wasanii, Kibao Kipya Cha Willy Paul

Marion Bosire

Kipindi Cha Wendy Williams Kuendelezwa na Watangazaji Tofauti

Marion Bosire

“Upendo” Kibao Kipya Kutoka Kwa Zuchu Na Spice Diana

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi