Hillary Barchok: Majani chai ya Bomet kuuzwa moja kwa moja nchini Iran

Gavana wa kaunti ya Bomet, Hillary Barchok, amewapuuzilia mbali wakosoaji wanaopinga uuzaji wa majani chai moja kwa moja kwa jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Barchok ambaye aliongoza ujumbe uliozuru Iran Juma lililopita, kufuatilia taratibu za kuuza majani Chai moja kwa moja katika taifa hilo, alisema nchi hiyo inawapa wakulima faida nzuri, kwa kulinganisha na bei zilizoko sasa kwenye solo la mnada wa majani chai la Mombasa.

Also Read
Munya ashtumiwa kufuatia mageuzi ya sheria za sekta ya kilimo

Alihimiza wizara ya kilimo kuunga mkono hatua hiyo ikizingatiwa kwamba masoko ya tangu jadi sasa yanakabiliwa na changamoto.

Also Read
Waziri wa Kilimo Peter Munya aridhishwa na juhudi za kukabiliana na nzige

Awali, waziri wa kilimo, Peter Munya, alikuwa amesema hakuna majani Chai yoyote kutoka Bomet tyanayouzwa moja kwa moja katika nchi ya Iran, huku akimshtumu gavana huyo kwa kuwadanganya wakulima  wa majani Chai.

Also Read
Afueni kwa Sakaja baada ya Mahakama kumuidhinisha kuwania Ugavana wa Nairobi

Wanachama wa buneg la kaunti ya Bomet walimtaka waziri Peter Munya, kuomba radhi kwa kutoa madai ya uwobngo kuhusu mauzo ya majani Chai ya moja kwa moja, baada ya shehena ya kwanza kupokewa huko Iran.

  

Latest posts

Wateja Milioni nne wa Fuliza kuondolewa kutoka CRB

Tom Mathinji

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi