Historia ya Mashemeji Derby kati ya AFC Leopards na Gor Mahia FC

Gor Mahia maarufu kama Ko galo na Afc Leopards almaarufu Ingwe watakuwa wakimenyana Jumapili hii Mei 8 katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani ikiwa mechi nambari 94 kati ya mahasimu hao wa tangu jadi kwa derby ya Nairobi ambayo ilibali jina na kuitwa derby ya Mashemeji , kutokana na uhusiano wa karibu kifamilia na kitabaka kati ya Ingwe iliyo na wafuasi wengi wa asili ya Abaluhya na Gor iliyoa na idadi kubwa ya wafuasi kutoka koo ya Dholuo.

Katika mechi ya Jumapili Gor ukipenda The green Army ambao walishinda ligi kuu kwa mara ya mwisho msimu wa mwaka 2019-2020, ndio itakuwa timu ya nyumbani nao Ingwe wawe ugenini ,mchuano ukiwa wa kuwania alama 3 muhimu za ligi kuu ya Kenya.

Also Read
Harambee Stars wataanzia wapi baada ya kubanduliwa kufuzu kombe la dunia na AFCON mwaka ujao?

Uhasama kati ya timu hizi mbili ulianza miaka mingi na mikaka iliyopita Derby ya kwanza ikisakatwa Mei 5 mwaka 1968 ,wakati huo pambano likisakatwa katika uwanja wa City jijini Nairobi.

Mechi hiyo ya mwaka 1968 ilikuwa ya kwanza kwa Gor Mahia kucheza baada ya klabu hicho kubuniwa ,kufuatia hatua ya kuziunganisha timu za Luo Union FC na Luo Stars FC na Gor Mahia wapata ushindi wa goli moja kwa ombwe.

 

Sio tu matokeo bali mechi kati ya timu hizi mbili ambao ni miamba wa soka nchini ,,imekuwa ikikumbwa na madai ya matumizi ya uchawi,visa vya vurumai mashabiki wakishambuliana au pia hata mechi kutibuka kwa wakati miwngine .

Baadhi ya itakadi za kishirikina zilizoshuhudiwa katika derby hii awali ni pamoja na wachezaji wa Leopards kudinda kutumia vyumba vya kubadilisha mavazi katika uwanja wa Nyayo kwa madai kuwa wapinzani wao Gor walikuwa wameficha maiti kwenye chumba hicho usiku wa kabla ya mechi,na pia wakati mmoja kichwa cha kuku kikapatikana uwanjani na kumbidi mwamuzi kusitisha mechi atupe kichwa nje ya uwanja ndiposa pambano likaendelea.

Also Read
Makundi ya wakiritimba yalaumiwa kwa kuficha Mahindi

Wakati mmoja pia mashabiki wa timu hizo walionekana kuwapulizia marefarii vumbi kabla ya mechi kuanza ikiaminika kuwa ushirikina na pia mechi kadhaa zimekosa kukamilika,mashabiki kuzua vurugu na kuwalazimu polisi kurusha vitoa machozi ili kuwatawanyisha.

Sio tu visa vya kihuni bali pia mashabiki hawa wamekuwa wakihubiri amani kwa wakati mwingi kabla ya mechi ambapo wamekuwa wakikutana katikati ya jiji la Nairobi kuimba, kupiga densi na hata kula chakula pamoja kabla ya kuelekea uwanjani.

Also Read
FKF yalalama kuhusu kukosekana kwa viwanja nchini

Pambano hili huwa na msisimuko wa kipekee sio tu alama tatu au kuwania kombe bali ,mshindi hujipatia haki za majitapo na kujigamba kuwa ndio mafundi wa soka.

Katika mechi ya Jumapili kuanzia saa tisa alasiri katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani,mashemeji derby inajiri wakati ambapo timu zote hazina uwezo wa kunyakua ubingwa wa ligi kuu msimu huu,Gor ikiwa ya tano kwa alama 46 ,wakati Leopards ikikalia nafasi ya 11 kwa pointi 38.

Gor Mahia imetawala derby 10 zilizopita na ushindi wa pekee wa Ingwe ukiwa mwaka 2016 mwezi Machi.

Jumapili  hii nani   mkali  ? Shemeji bora na aibuka na ushindi.

  

Latest posts

IEBC kutangaza rasmi matokeo ya Urais Jumatatu

Dismas Otuke

Andrew Mwadime ndiye Gavana mpya wa Taita Taveta

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 12 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi