Hofu yatanda Busia baada ya mfanyibiashara mashuhuri Alfred Obayo kuuawa kwa kupigwa risasi

Biwi la simanzi limegubika jamii ya wafanyibiashara wa Mji wa Busia baada ya mwanyibiashara mmoja mjini humo, Alfred Olu Obayo, kuuawa kwa kupigwa risasi.

Obayo mwenye umri wa miaka 60, ambaye alikuwa mmiliki  wa hoteli ya Texas Annex katika mji wa Busia, aliuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana katika hoteli yake saa tatu usiku wa Jumatatu.

Mwenyekiti wa Chama cha Kitaifa cha Biashara na Viwanda katika Kaunti ya Busia, Silvanus Abungu, ametuma salamu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu Obayo na ametoa wito kwa vyombo vya usalama kuharakisha uchunguzi kuhusiana na mauaji hayo.

Also Read
Chifu mmoja ampiga na kumuua nduguye huko Teso

Akithibitisha mauaji hayo, Kamanda wa Polisi wa Kaunti ya Busia, John Nyoike ambaye alizungumza na Shirika la Utangazaji Nchini (KBC) kwa njia ya simu, amesema washambuliaji wawili walikwenda kwenye hoteli ya mwendazake wakijifanya wateja lakini ghafla mmoja wao akatoa bunduki na kumpiga risasi na kumuua mfanyabiashara huyo.

Also Read
Watu kadhaa wahofiwa kufariki kwenye ajali ya moto Busia

Nyoike amesema hakuna kilichoibiwa kutoka kwa marehemu na kuongeza kuwa Idara ya Upelelezi kuhusu Uhalifu huko Busia wameanzisha uchunguzi.

Afisa huyo wa Polisi ametoa wito kwa umma kujiepusha na uvumi kuhusu kiini cha mauaji hayo na badala yake kuwapa fursa maafisa wa upelelezi kuendesha uchunguzi.

Also Read
Wakili wa Sonko kwenye kesi ya ufisadi ajiondoa

Nyoike pia amehimiza yeyote ambaye ana habari ambazo zinaweza kusaidia polisi katika uchunguzi kuzitoa kwa polisi.

Amewahakikishia wafanyabiashara usalama wao na kukariri kuwa polisi watafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kuwa waliohusika wametiwa mbaroni.

Marehemu alikuwa Mkurugenzi wa Fedha wa tawi la Kaunti ya Busia la chama cha Kitaifa cha wafanyabiashara na wenye Viwanda nchini.

  

Latest posts

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Watu watano wana kesi ya kujibu dhidi ya mauaji ya wakili Willie Kimani

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi