Hoja ya kumng’atua Spika wa kaunti ya Tana River yaidhinishwa

Wanachama wa bunge la kaunti ya Tana River wameidhinisha kwa kauli moja hoja ya kumwondoa mamlakani spika wao Michael Nkaduda.

Hoja hiyo iliyowasilishwa na mwakilishi wa wadi ya Mikinduni Muhammed Buya Yusa, inamshutumu spika huyo kwa utepetevu, utumiaji mbaya wa mamlaka na mienendo isiyofaa.

Also Read
Wanawake Tana River wajitosa kutetea nafasi za uongozi serikalini

Aidha wawakilishi hao wa wadi wanadai kwamba spika huyo anawanyima wakazi fursa ya kuingia katika afisi za bunge na kuwafukuza wanachama wa bunge la kaunti hiyo kwenye afisi zao.

Also Read
Bei ya mafuta yaongezwa hapa nchini

Musa Wario, ambaye ni mwakilishi wadi wa Garsen magharibi, anadai kwamba spika anajihusisha na kampeni za mapema kwa kutumia magari ya bunge la kaunti hiyo.

Vile vile wanadai kwamba anakiuka katiba kwa kuruhusu mswada wa mradi wa maridhiano-BBI ujadiliwe bila ushiriki wa umma.

Also Read
Mung’ara Githinji wa Jubilee ashinda uchaguzi mdogo wa Wadi ya Mugugua

Wanachama hao wa bunge la kaunti sasa wamebuni kamati ya wanachama 10 kumchunguza spika huyo na kuwasiliwsha ripoti kwa bunge hilo wiki ijayo.

  

Latest posts

Visa 394 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Chris Obure ana kesi ya kujibu kuhusiana na sakata ya Anglo Leasing

Tom Mathinji

Rais Kenyatta atoa wito wa kuongezwa kwa uwekezaji wa Kilimo

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi