Homeboyz wazima kelele za Sirkal baada ya kuwapiga kumbo 2-1

Rekodi ya Gor Mahia kutoshindwa mechi msimu huu kligini imefutwa Jumamosi jioni baada ya kucharazwa mabao 1-2 na Kakamega Homeboyz katika uga wa Bukhungu kaunti ya Kakamega.

Gor walikuwa wa kwanza kupachika bao kunako dakika ya 3 kupitia kwa Peter Lwasa,kabla ya George Odiwour kusawazisha kupitia mkwaju wa penati na kipindi cha kwanza kumalizikia sare ya 1-1.

Also Read
Tume ya usawa na jinsia yataka sheria kupitishwa kukabiliana na dhuluma za kijinsia

Homeboyz walijizatiti kipindi cha pili ndiposa mshambulizi wa Tanzania Stephen Opoku akapachika goli la pili na ushindi.

Also Read
CAF yakubali ombi la Gor na kuahirisha mechi ya ligi ya mabingwa hadi Jumamosi

Matokeo hayo yameipaisha Homeboyz hadi nafasi ya pili kwa alama 21 sawa na viongozi KCB,huku Gor wakishuka hadi nambari tatu kwa pointi 18.

Also Read
Tusker Fc wapangwa dhidi ya AS Arta Solar 7 ya Djibouti huku mshindi akipamabana na Zamalek katika ligi ya mabingwa Afrika

Homeboyz ndio timu pekee ambayo haijashindwa ligini msimu huu.

Katika matokeo mengine Sofapaka walilaziimisha sare ya 1-1 nyumbani Wundanyi dhidi ya Posta Rangers nao wanajeshi Ulinzi Stars wakaikomoa Vihiga Bullets 2-0.

  

Latest posts

Andrew Mwadime ndiye Gavana mpya wa Taita Taveta

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 12 zaidi vya Covid-19

Tom Mathinji

Familia ya afisa wa IEBC aliyetoweka yazungumza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi