Huduma ya Polisi yawahimiza wakenya kudumisha amani

Inspekta Jenerali wa polisi Hillary Mutyambai, amewapongeza wakenya kwa kudumisha amani wakati wa kipindi ambacho kimekamilika cha Uchaguzi Mkuu.

Kupitia kwa taarifa, huduma ya taifa ya polisi ilitoa wito kwa wakenya kudumisha amani na kuzingatia sheria baada ya Uchaguzi Mkuu.

Wito huo wa huduma ya taifa ya polisi, ulitolewa baada ya kutangazwa kwa matokeo ya kura za urais siku ya Jumatatu Jioni na tume huru ya Uchaguzi na Mipaka IEBC.

Also Read
Naibu Gavana wa Makueni Adelina Mwau ajiunga na chama cha UDA

Aidha matokeo hayo yaliyomtangaza William Ruto kuwa Rais Mteule, yalipingwa na mshindani wake wa karibu Raila Odinga wa muungano wa Azimio, huku makamishna wanne wa tume ya IEBC wakijitenga na matokeo hayo.

Ghasia zilizuka katika ukumbi wa Bomas kabla ya kutangazwa kwa matokeo hayo na kusababisha kujeruhiwa kwa makamishna wawili wa IEBC, pamoja na afisa mkuu mtendaji  Marjan Hussein Marjan. Maafisa wa polisi waliingilia kati na kutuliza hali.

Also Read
Mahakama: BBI ni kinyume cha sheria

Huduma hiyo ya taifa ya polisi, ilisema tume huru ya Uchaguzi na mipaka, imetekeleza wajibu wake wa kikatiba, kwa kutangaza matokeo ya kura za Urais.

“Huduma ya taifa ya polisi inawapongeza wakenya kwa kutekeleza haki zao za kikatiba ya kupiga kura. Tunawashukuru pia wakenya kwa kudumisha amani na utulivu tangu siku ya upigaji kura hadi sasa,” ilisema huduma ya taifa polisi.

Also Read
Wazazi wa watoto wenye ulemavu wahimizwa kutowabagua

Kutangazwa kwa matokeo ya kura za Urais kuliibua hisia mseto, huku wafuasi wa Ruto wakisherehekea na wale wa Raila wakigadhabishwa na matokeo hayo na wakimhimiza Raila kupinga matokeo hayo mahakamani.

Ruto alipata jumla ya kura 7,176,141, hii ikiwa ni asilimia 50.49, naye Odinga alipata kura 6,942,930, ikiwa ni asilimia 48.85 ya kura zilizopigwa.

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi