Huenda marufuku ya usafiri yakarejeshwa hapa nchini kudhibiti msambao wa Covid-19

Huenda Serikali ikarejesha marufuku ya kusafiri ili kuzuia msambao wa virusi vya Covid-19 vinavyoongezeka kila uchao humu nchini.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya kanisa la Kianglikana humu nchini katika kanisa la All Saints Cathedral jijini Nairobi, Rais Uhuru Kenyatta alifichua kwamba serikali inachunguza kwa makini hali ya ugonjwa wa COVID-19 humu nchini kabla ya uamuzi wa mwisho kuafikiwa.

Also Read
Mututho ataka Bunge lipitishe mswada wa kukabiliana na mihadarati

Hata hivyo alikariri haja iliyopo kwa kila Mkenya kuzingatia kwa dhati kanuni za kuzuia msambao wa ugonjwa wa COVID-19 ili kukomesha maambukizi huku kukiwa na hofu ya kuzuka kwa wimbi la pili la maambukizi.

Also Read
Visa 719 vipya vya Covid-19 vyanakiliwa huku watu 8 zaidi wakifariki hapa nchini

Alidokeza kuwa wimbi la pili la maambukizi ya Covid-19 liko nasi na limesababisha serikali kuchunguza iwapo litarejesha masharti yaliyokuwepo ya kukabiliana na Covid-19.

Kiongozi wa Kanisa la Kianglikana humu nchini Dkt Jackson Ole Sapit, akiongea katika ibada hiyo,alitoa wito kwa Rais Uhuru Kenyatta kusitisha mikutano yote ya kisiasa kote nchini akitaja mikutano hiyo kuwa tisho kwa taifa hili.

Also Read
Kuahirisha chaguzi za Afrika kwafaa licha ya mizozo ya kikatiba asema Dkt Matsanga

Kanisa la Kianglikana lilifikisha miaka 50 tarehe 3 mwezi Agosti lakini sherehe hizo zikaahirishwa wakati huo kutokana na janga la Covid-19

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi