Idadi ndogo ya wakazi wa Nairobi wajitokeza kuchanjwa dhidi ya COVID-19

Maafisa wa wizara ya afya kutoka kaunti ya Nairobi wameelezea masikitiko yao kuhusiana na idadi ndogo ya watu wanaojitokeza kupata chanjo dhidi ya COVID 19.

Hatua hiyo inatokana na hatua ya baadhi ya wakazi wa Nairobi ya kuchagua chanjo ama kusita kuchanjwa dhidi ya COVID-19.

Kulingana na afisa wa afya wa shirika la utoaji huduma katika Jiji la Nairobi NMS,Teresia Mukono, baadhi ya wale wanaojitokeza kupata chanjo dhidi ya COVID-19, wanaamua kusita dakika za mwisho ikiwa aina ya chanjo wanayohitaji haipo.

Mukono aliwahakikishia wananchi kwamba chanjo zote ni salama na kwamba hakuna ilio-bora kuliko ingine.

Kaunti ya Nairobi inafanya chanjo ya watu wengi itakayodumu kwa muda wa siku tatu na inawalenga wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma.

Shughuli hiyo ilioanza siku ya Ijumaa inatarajiwa  kukamilika siku ya Jumapili.

Kufikia sasa, watu milioni 3.33 kote nchini wamepata chanjo dhidi ya COVID-19 huku shirika la utoaji huduma kwa jiji la Nairobi likilenga kutoa chanjo kwa wakazi milioni 2.5 wa Nairobi kufikia mwisho wa mwaka huu.

  

Latest posts

Watu 25 zaidi wameambukizwa Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Kongamano la Ma-jiji lafunguliwa rasmi Jijini Kisumu

Tom Mathinji

Wanjigi amteua Willis Otieno kuwa mgombea mwenza wake

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi