Idadi ya mimba za mapema yazidi kuongezeka Pokot Magharibi

Idadi ya wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shulen inazidi kuongezeka katika kaunti ya Pokot Magharibi, huku shule ya msingi ya wasichana ya Alale ikiongoza ambapo wanafunzi 50 ambao wana watoto.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo Pamela Oluoch, alisema wengi wa wasichana hao ambao wana watoto tayari wamerejea shuleni kuendelea na masomo.

kwa mujibu wa mwalimu huyo mkuu, wasichana wengi baada ya kuolewa, mzigo wa maisha uliwalemea na wakaazimia kurejea shuleni. Pamela alipongeza jamii ya wa- Pokot kwa kukumbatia elimu licha ya kukumbwa na changamoto nyingi kama vile mimba za mapema na maisha ya kuhamahama.

Also Read
Wakazi wa Pokot Magharibi na Trans Nzoia kupokea nguvu za umeme zisizokatizwa

Hatua za wanafunzi hao kurejea shuleni alisema ziliwezeshwa na juhudi za kuwatafuta wasichana hao punde wanapokosa kuenda shuleni, ambapo wazazi wa wasichana hao hupigiwa simu wawapeleke watoto wao shuleni.

Also Read
Chebet atuzwa mwanaspoti bora wa LG/SJAK mwezi April

Mwalimu huyo mkuu alitoa wito kwa wasamaria wema kuwasaidia wasichana hao waliopata watoto kuendelea na elimu yao.

Kulingana na mwalimu huyo, jangala Covid-19 lilisababisha idadi ya wasichana wanaoenda shuleni kupungua kutoka wasichana 300 hadi wasichana 200.

Gloria Chemsutut aliye na umri wa miaka 27, alirejea shuleni baada ya kujifungua watoto watatu. Chemsutut alikuwa amecha shule mwaka 2013.

Also Read
Watu 24 wafariki kutokana na makali ya Covid-19 huku visa 1,344 vipya vikinakiliwa nchini

Mshirikishi wa afya ya uzazi katika kaunti ya Pokot Magharibi Wilson Ngareng, alisema mpango wa upangaji uzazi umeongezeka katika kaunti hiyo, utoka asilimia 15 hadi asilimia 25 katika muda wa miaka mitatu iliyopita.

  

Latest posts

Shikanda ahifadhi uenyekiti wa AFC Leopards

Dismas Otuke

Kalle Rovanpera atwaa ubingwa wa raundi ya Kenya mashindano ya WRC

Tom Mathinji

Ajali ya kwanza yatokea katika barabara ya Expressway

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi