Idara ya magereza yawatuza washiriki wake wa Olimpiki

Idara ya magereza imewatuza maafisa wake 14 walioshiriki makala ya 32 ya michezo ya Olimpiki iliyokamilika maajuzi mjini Tokyo Japan.

Kwenye hafla iliyoandaliwa mapama Alhamisi katika makao makuu ya magereza, Kamishna mkuu  wa magereza Willy Ogallo ameahidi kuwa wataendelea kutambua na kukuza vipaji vya michezo, huku akiwapongeza maafisa hao 14 kwa kujitolewa kuiwakilisha nchini kwenye michezo hiyo ya Tokyo.

Also Read
Mali waipakata Burkina Fasso 1-0 CHAN

 

Kamishna mkuu wa magereza Wycliff Ogalo kwenye picha washiriki wa Olimpiki

 

“Tutaendelea kusajili wanamichezo katik idara yetu kama njia ya kukuza talanta,pia nawahimiza wanamichezo wa magereza kujituma zaidi na kuchukua kozi za mafunzo ambazo zitawapa ujuzi wa kujitegemea baada ya kustaafu ”

Also Read
Faith Ogalo atimiza ndoto ya miaka 12 ya Kenya kutuma mshiriki kwa michezo ya Olimpiki katika Taekwondo

Miongoni mwa waliotuzwa kwenye hafla hiyo ni mshindi wa nishani ya fedha ya Olimpiki katika mita 1500 Inspekta mkuu Timothy Cheruiyot, Setter wa timu ya taifa ya Voliboli Jane Wacu,  Lillian Kassait na wengineo.

Also Read
Uingereza yaruhusu tena mashabiki viwanjani

Kwa Jumla idara ya magereza ilikuwa na wachezaji 9 wa Voliboli katika timu ya taifa iliyokuwa Olimpiki, wanariadha watatu na maafisa wawili.

  

Latest posts

Bayern Munich wapokea kichapo cha kihistoria 5-0 dhidi ya Borusia Monchengladbach na kutemwa nje ya kombe la DFB

Dismas Otuke

Ronald Koeman atimuliwa Barcelona baada ya kushindwa na Vallecano

Dismas Otuke

Droo ya Safari Sevens yatangazwa Mabingwa watetezi Morans wakikutanishwa na Uhispania

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi