Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa yaonya kuhusu kiangazi Januari

Wakenya wameshauriwa kujiandaa kwa hali ya kiangazi mwezi Januari mwaka wa 2021.

Taarifa kwa vyumba vya habari iliyotiwa saini na Dkt. Richard Muita kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini, inasema hali hiyo ya kiangazi ni kutokana na viwango vya chini vya joto katika maeneo ya katikati kuelekea Mashariki mwa Bahari ya Pacific, na viwango vya juu vya joto katika maeneo ya Magharibi mwa bahari hiyo, hii ikiashiria mfumo wa hali ya hewa wa La NiƱa.

Also Read
Migogoro kati ya binadamu na wanyamapori yaongezeka kaunti ya Homa Bay

Hali hii kwa kawaida husababisha upungufu wa mvua nchini Kenya.

Dkt. Muita anasema hali hiyo ya kiangazi huenda ikasababisha uhaba wa maeneo ya malisho ya mifugo na pia wanyama pori.

Aidha, amesema hali hiyo huenda ikasababisha uhaba wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani na pia mifugo na kuchochea migogoro popote ambako kutakuwa na uhaba wa bidhaa hiyo.

Also Read
Maskwota wa Kilifi kupewa makazi na Serikali

Ameongeza kwamba mwanzo wa mvua za Masika, hususan mwezi Mei, huenda ukaandamana na mafuriko katika maeneo ya nyanda za chini na pia kwenye kingo za mito inayomimina maji yao kwenye Ziwa Victoria, sawia na maeneo mengine yanayozunguka maziwa ya Rift-Valley.

Kutokana na hali hiyo, idara ya utabiri wa hali ya hewa nchini imeshauri Wizara ya Usalama wa Kitaifa na taasisi za kutoa misaada ya kibinadamu kuratibu mikakati ya kuepusha hali zinazoweza kusababisha vifo, kupotea kwa njia za kujipatia riziki na pia mali za watu.

Also Read
Vitambulisho kufutiliwa mbali Disemba kwa ajili ya kadi za Huduma Namba

Hata hivyo, maeneo mengi ya humu nchini yanatarajiwa kupokea mvua kuanzia Alhamisi hadi tarehe 3 Januari, hivyo Wakenya wameshauriwa kuratibu njia za kuvuna na kuhifadhi maji.

  

Latest posts

Nyongeza ya bei za mafuta yapingwa Mahakamani

Tom Mathinji

Kenya yanakili visa 113 vipya vya COVID-19

Tom Mathinji

Wazazi wasema watatetea mtaala mpya wa Elimu wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi