IEBC kusajili zaidi ya wapiga kura 4,000 wapya Kilifi

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini (IEBC) inalenga kusajili zaidi ya wapiga kura wapya 4,000 wakati wa zoezi linaloendelea la kuelimisha umma kuhusu maswala ya upigaji kura katika Kaunti ya Kilifi.

Akihutubia waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo katika afisi za IEBC mjini Kilifi, Mkuu wa tume hiyo katika kaunti ya Kilifi Abdul Wahid Hussein alisema tume hiyo inanuia kuhamasisha wakazi kuhusu mchakato wa upigaji kura.

Also Read
Afueni baada ya tume ya kudhibiti kawi kupunguza bei za mafuta nchini

Kulingana na Hussein, wakazi wengi wa Kilifi huwa wanasusia zoezi la usajili wa wapiga kura licha ya kuwa kaunti kubwa zaidi katika eneo la Pwani, huku Kaunti Ndogo ya Malindi ikiwa na idadi ndogo zaidi.

Also Read
Serikali yahimizwa kupunguza ushuru kwa sekta ya Utalii ili kuimarisha utalii wa nyumbani

“Kilifi ndiyo kaunt kubwa zaidi Pwani lakini wakazi hawajitokezi kwa zoezi hilo. Tuko na takriban wapiga kura nusu milioni tu. Tangu mwaka wa 2017, tumesajili wapiga kura 11,000 zaidi. Kuna sehemu nyingi sana ambazo watu wengi hawajaandikishwa,” akasema afisa huyo.

Naibu Gavana wa kaunti hiyo Gideon Saburi pia alihudhuria hafla ya uzinduzi wa zoezi hilo na kuwarai wakazi wajisajili kama wapiga kura kwa wingi ili waweze kufanya maamuzi ya busara katika uchaguzi mkuu ujao.

Also Read
Kenya yajiunga na nchi zingine kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika

“Tunataka kuhakikisha kwamba watu wanaelewa umuhimu wa upigaji kura. Ni muhimu kwamba wahamasishwe ili watambue kwamba kupiga kura ni haki yao,” akasema Saburi.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Bwawa katika mto Nile lazidisha uhasama kati ya Ethiopia, Sudan na Misri

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi