IEBC kutangaza rasmi matokeo ya Urais Jumatatu

Tume huru ya mipaka na uchaguzi nchini IEBC, inatarajiwa kutangaza matokeo ya kura za Urais Jumatatu Adhuhuri .

Tayari mchakato wa kujumuisha matokeo ya kura za Urais , kutoka maeneo bunge yote 290 na eneo la ughaibuni lilikamilishwa mapema Jumatatu na maafisa wa IEBC.

Taifa limekuwa katika hali ya taharuki huku mshindi atakayetangazwa,  akitarajiwa kuwa aidha Raila Odinga wa muungano wa Azimio One Kenya Alliance au William Ruto wa chama cha United Democratic Alliance.

Kisheria mshindi wa Urais ni sharti atimiza asilimia 50 na kura moja ya idadi ya kura zote ,na pia ni sharti apate asilimia 25 katika kaunti zaidi ya 24 ,kati ya kaunti 47.

Endapo hakutakuwa na mshindi IEBC itaandaa uchaguzi upya baina ya waaniaji wawili wa kwanza ndani ya siku 60.

Ikiwa kutakuwa na mshindi katika raundi ya kwanza ,sheria inatoa siku 30 za kusikizwa na kuamuliwa kwa kesi ya kupinga matokeo ya kura za Urais na mahakama ya upeo.

Endapo hakutakuwa na kesi ya kupinga matokeo ya Urais ,Rais mteule ataapishwa Agosti 30 mwaka 2022 akipokezwa mamlaka na Rais anayeondoka Uhuru Kenyatta.

 

  

Latest posts

Wetangula kuamua Alhamisi ni chama kipi kitashikilia wadhifa wa kiongozi wa wengi bungeni

Tom Mathinji

Gavana Orengo awatuma maafisa wakuu wa kaunti kwa likizo ya lazima

Tom Mathinji

Kipchoge na Kipruto warejea nyumbani kutoka London

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi