IEBC, ODP na EACC kushirikiana na vyombo vya habari ili kukuza uwazi

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati, Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma, Noordin Haji na  Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, Twalib Mbarak, wamejitolea kufanya kazi kwa karibu na vyombo vya habari, katika uchaguzi mkuu ujao.

Also Read
Wakazi wa Busia wahimizwa kujisajili kuwa wapiga kura

Wanasema kufanya kazi na vyombo vya habari kutasaidia katika kusambaza habari sahihi kwa raia.

Walisema hayo kwenye  mkutano wa kundi la wadau wa Sekta ya Habari unaoendelea huko Diani, Kaunti ya Kwale.

Kulingana na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka, Wafula Chebukati, tume hiyo itafanya kazi na vyombo vya habari, ili kuongeza uwazi wa michakato ya uchaguzi na kuhakikisha uwajibikaji wa matokeo ya uchaguzi kutoka vituo vya kupigia kura.

Also Read
Haji akabidhi ripoti ya uchunguzi wa KEMSA kwa Tume ya EACC
Also Read
Magoha: Serikali haitabatilisha agizo lake kuhusu utumiaji wa mabasi ya shule.

Hata hivyo, viongozi hao watatu waliongeza kuwa vyombo vya habari vinapaswa kuchukua jukumu muhimu katika kuhakikisha usajili wa wapiga kura, na utoaji wa  elimu  kwa wapiga kura, kwa kutoa gharama  nafuu ya  matangazo kwa tume hiyo ya uchaguzi.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi