IEBC yaandaa zoezi la upigaji kura la muigo katika ukumbi wa Bomas

Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka hapa nchini  IEBC, siku ya Jumapili alasiri iliandaa zoezi la muigo wa upigaji kura,  kabla ya kuandaliwa kwa Uchaguzi Mkuu wa siku ya Jumanne ili, kuhakikisha mchakato mzima wa upigaji kura uko shwari.

Makamishna saba wa tume ya IEBC na baadhi ya wahudumu wa tume hiyo, walishiriki kwenye zoezi hilo la mwigo. Kamishna Boya Mulu alisema shughuli hiyo ya elimu kwa wapiga kura inanuiwa kuwaelimisha WaKenya kuhusu mchakato wa upigari kura.

Also Read
Justin Muturi: Miungano mikubwa ya kisiasa haipaswi kuhujumu vyama vidogo vya kisiasa

Tume hiyo iliiga hali mbali mbali ambazo huenda zikajitokeza mnamo siku ya Uchaguzi Mkuu. Mwenyekiti wa tume hiyo Wafula Chebukati alikuwa wa kwanza kupiga kura kwenye zoezi hilo la muigo katika ukumbi wa Bomas Jijini Nairobi.

Also Read
Maoni zaidi ya wananchi yahitajika kutaifisha Kenya Airways
IEBC yaandaa zoezi la upigaji kura la muigo, katika ukumbi wa Bomas.

Kwenye shughuli hiyo, tume ya IEBC iliiga hali ambapo mpiga kura huenda akataka kumpigia kura Rais pekee.

Also Read
Serikali itatumia shilingi bilioni moja kufufua sekta ya Pareto nchini

Vituo 46, 232 vya kupigia kura vitatumiwa kwenye uchaguzi siku ya Jumanne. Kila kituo cha kupigia kura kitatumiwa wakati wa uchaguzi huo. Kila kituo kitakuwa na jumla ya wapiga kura 700 waliosajiliwa.

  

Latest posts

Maendeleo ya Wanawake yampongeza Rais kwa kuwateuwa wanawake mawaziri

Dismas Otuke

NMS yakabidhi majukumu yake kwa kaunti ya Nairobi

Tom Mathinji

KBC Channel One na Idhaa 13 kupeperusha mechi za kipute cha kombe la dunia

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi