IEBC yakanusha kuwa mifumo yake imedukuliwa

Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imekanusha ripoti kwenye  baadhi ya vyombo vya habari kuwa  mtu mmoja amedukua mifumo yake na kupata maelezo ya kibinafsi ya wapiga kura waliosajiliwa kutoka kaunti za Magharibi mwa nchi hii.

Taarifa iliyotiwa saini na Mwenyekiti wa Tume hiyo Wafula Chebukati, ilisema sajili ya tume hiyo imehifadhiwa katika mfumo wa Usajili wa Wapiga kura wa Biometrik  (BVR) uliowekwa kwenye sava kadhaa na  kwenye mtandao  uliotengwa na   akaunti za  wapiga kura  ili kuhakikisha uadilifu na kuhifadhiwa siri.

Chebukati anasisitiza kuwa mfumo  huo hauwezi kudukuliwa kwa kuwa haujaunganishwa na  mitandao iliyo  wazi na una mfumo wa usalama wa hali ya juu. 

Hata hivyo,  Chebukati anakubali kwamba  takwimu   zinazohusika zingeweza kutafutwa kihalali na mashirika fulani baada ya kulipa ada kwa tume hiyo.

Ijumaa iliyopita mshukiwa mmoja wa ulaghai alikamatwa akiwa mamia ya kadi za simu za  Safaricom, Airtel na kampuni zingine za mawasiliano.

Also Read
Rais Kenyatta akagua miradi mbali mbali ya maendeleo
Also Read
Bunge kuanza kujadili mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020

Kwa mujibu wa majasusi takwimu zilizopatikana zilijumuisha majina ya wapiga kura,nambari za vitambulisho,na tarehe za kuzaliwa zinazodaiwa kutolewa kwa mifumo ya IEBC.

  

Latest posts

Justin Muturi kuwania urais kwa tiketi ya chama cha DP

Tom Mathinji

Bunge lapendekeza kuchunguzwa kwa mfumo wa ununuzi wa KEMSA

Tom Mathinji

Serikali yatoa chakula cha msaada kwa wanaokabiliwa na njaa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi