IEBC yalenga kuwasajili wapiga kura wapya milioni sita kabla Uchaguzi Mkuu ujao

Tume huru ya uchaguzi na mipaka-IEBC kuanzia tarehe 4 mwezi ujao itazindua shughuli endelevu ya usajili wa wapiga kura unayowalenga wapiga kura milioni sita ambao hawajasajiliwa hasa vijana wenye umri wa miaka 18 na zaidi walio na vitambulisho vya kitaifa.

Kwenye taarifa mwenyekiti wa tume ya IEBC, Wafula Chebukati pia alikariri kwamba uchaguzi mkuu utaandaliwa tarehe 9 mwezi Agosti mwaka ujao akisema kwamba mpango wa kusimamia uchaguzi ulioratibiwa na tume hiyo tarehe 15 mwezi Juni unazingatia tarehe hiyo.

Also Read
Kamati ya BBI yawasilisha saini milioni 4.4 kwa IEBC

Alisema tume hiyo inafahamu kuhusu kesi zilizoko mahakamani za kutaka kubadilishwa tarehe ya uchaguzi lakini akasema hakuna maagizo ya mahakama yanayozuia tume hiyo kufanya matayarisho ya uchaguzi mkuu.

Also Read
Chebukati: Hatukusambaza nakala tofauti za mswada wa marekebisho ya Katiba

“Kama tume ya uchaguzi, tunafahamu kuwepo kwa kesi mahakamani, lakini hakuna maagizo ya mahakama ya kuzuia maandalizi ya uchaguzi mkuu,” alisema Chebukati.

Also Read
Mikakati yawekwa kuhakikisha usalama katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022

Chebukati hata hivyo alisema kwamba kuna changamoto ambazo zinaendelea kukumba tume hiyo  kama vile idadi kubwa ya makamishna na wafanyikazi, kuchelewa kupitishwa sheria za uchaguzi, kesi kadhaa zilizoko mahakamani na maamuzi ya mahakama yanayotolewa uchaguzi unapokaribia.

  

Latest posts

Idara ya Mahakama yashutumiwa kwa kuhujumu shughuli muhimu za serikali

Tom Mathinji

Uhuru Kenyatta: Usalama wa taifa hili ni shwari

Tom Mathinji

Hospitali ya Kijeshi yazinduliwa katika kambi ya kijeshi ya Kahawa

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi