IEBC yasimamisha ujumuishaji wa kura katika eneo bunge la Juja kufuatia vurugu

Shughuli ya ujumlishaji wa kura haijaanza katika eneo bunge la Juja baada ya shughuli hiyo kusimamishwa kwa muda jana usiku baada ya vurugu kutokea.

Kwenye taarifa, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati alimlaumu Gavana wa Kiambu James Nyoro kwa kutibua shughuli ya ujumuishaji wa kura kwenye kituo hicho cha Mangú.

Also Read
Kituo cha utafiti wa ugonjwa wa Saratani chazinduliwa hapa nchini

Awali, watu watatu waliingia kwenye kituo hicho na kuzua rabsha. Hata hivyo polisi walifika hapo na kutuliza hali kwa kuwakamata watu hao.

Hata hivyo, vurugu zilizuka tena kati ya wafuasi wa mgombea wa chama ha Jubilee Susan Njeri wakiongozwa na Gavana Nyoro na mwakilishi wa wanawake wa Kiambu Gathoni waMuchomba na wafuasi wa mgombea wa chama cha Peoples Empowerment Paty-PEP George Koimburi, wakiongozwa na wabunge Moses Kuria, Ndindi Nyoro, Seneta Irungu Kang’ata na mwakilishi wa Wadi ya Witethie Julius Macharia.

Also Read
Kagwe: Habari za uwongo zinahujumu ufanisi katika sekta ya afya
Also Read
Waliowatunga mimba wasichana wa shule kutangazwa hadharani

Gavana Nyoo alidai kura za Njeri zilitupwa kwenye shule moja huko Juja na kutaka shughuli nzima ya ujumuishai kura kukomeshwa.

Wafuasi wa kiongozi wa wadi ya Witethie Julius Macharia walimlaumu Nyoro kwa kutumia majambazi kuvuruga shughuli hiyo ili kumfaa mgombea wa chama cha Jubilee.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Visa 511 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi