IEBC yatangaza tarehe ya chaguzi ndogo za Garissa, Bonchari na Juja

Chaguzi ndogo za useneta wa Garissa pamoja na zile za ubunge za Bonchari na Juja zitaandaliwa tarehe 18 mwezi Mei mwaka huu.

Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imesema uchaguzi mdodo wa wadi ya Rurii Kaunti ya Nyandarua pia utaandaliwa siku hiyo.

Hayo yanajiri baada ya maspika wa Seneti, Bunge la Kitaifa na la Kaunti ya Nyandarua kutangaza viti hivyo kuwa wazi kufuatia vifo vya waliokuwa viongozi wa maeneo hayo.

Also Read
Mahakama yaamuru kufidiwa kwa waliofurushwa kimakosa karibu na Uwanja wa Ndege wa Wilson

Kupitia taarifa iliyochapishwa kwenye Gazeti rasmi la serikali, tume hiyo amevitaka vyama vya kisiasa kuwasilisha orodha ya wale watakaoshiriki kwenye chaguzi zao za mchujo na tarehe ya mchujo kabla ya tarehe 8 mwezi mwezi huu.

Wale wanaotaka kuwania nyadhifa hizo kama wagombeaji huru wanatarajiwa kutokuwa mwanachama wa chama chochote kwa kipindi cha miezi mitatu kabla ya tarehe ya uchaguzi huo mdogo.

Kulingana na taarifa ya IEBC, muda wa kampeni wa chaguzi hizo utaanza tarehe 29 mwezi huu na kutamatika tarehe 15 mwezi Mei.

Also Read
Serikali yajipanga kukabiliana na wimbi la pili la uvamizi wa nzige

Haya yanajiri huku tume hiyo ikikamilisha matayarisho ya chaguzi ndogo za hapo kesho katika maeneo bunge ya Matungu na Kabuchai pamoja na wadi kadha.

Tume hiyo imesema kwamba maafisa wa kutosha wa usalama wamepelekwa katika vituo vya kupigia kura na kwamba shughuli hiyo itaandaliwa kwa kuzingatia maagizo ya kuzuia maambukizi ya virusi vya korona.

Akiongea na wanahabari pamoja na wachunguzi wa uchaguzi huo katika Eneo Bunge la Kabuchai Kaunti ya Bungoma, Kamishna wa IEBC Boya Molu amethibitisha kwamba tume hiyo itatoa barakoa kwa maafisa wote wa uchaguzi kulingana na maagizo ya kukabiliana na msambao wa ugonjwa wa COVID-19.

Also Read
Wakenya walio na uraia wa nchi zingine hawatateuliwa kuwa mabalozi

Tume ya uchaguzi imetoa wito kwa vyombo vya habari kuhakikisha vinachapisha habari sahihi kuhusu zoezi hilo.

Viti vya maeneo bunge ya Matungu na Kabuchai vilisalia wazi kufuatia vifo vya wabunge Justus Murunga na James Lusweti mtawalia.

  

Latest posts

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Kagwe: Watoto hawatachanjwa dhidi ya COVID-19

Tom Mathinji

Visa 511 vipya vya COVID-19 vyanakiliwa hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi