Ingwe wapokea ufadhili wa shilingi milioni 60 kutoka Spotika

Miamba wa soka nchini klabu ya AFC Leopards wamepokea ufadhili wa shilingi milioni 60 kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka kwa kampuni mpya ya kamari Spotika .

Kulingana na mkataba huo Spotika itakuwa mfadhili mkuu kwa Ingwe ambao ni mabingwa wa ligi kuu mara 12,huku mkataba huo ukianza kutekelezwa baada ya kung’oa nanga kwa msimu wa mwaka 2022 na 2023 wa ligi kuu nchini.

Also Read
Mwenyekiti wa zamani wa AFC Leopards Alex Ole Magelo afariki
Also Read
Mashemeji Ingwe na Kogalo kupimana nguvu fainali ya FKF CUP

Klabu hiyo itapokea shilingi milioni 20 kwa kila mwaka, katika kipindi cha miaka mitatu.

Ingwe wamekuwa wakipitia wakati mgumu kifedha baada ya wafadhili kampuni ya Betsafe kujiondoa mwishoni mwa msim jana.

Also Read
Ngoma ya Burna Boy last last yagonga views milioni 4 nukta 7 ndani ya siku 10 pekee

Hafla hiyo ya mapema Alhamisi ilihudhuriwa na waziri wa ulinzi Eugene Wamalwa,mkurugenzi katika idara ya uhamiaji Alex Muteshi,na mwenyekiti Dan Shikanda.

  

Latest posts

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Mabingwa wa dunia Ufaransa na Uingereza waangukia pua katika droo ya kufuzu kwa kombe la Euro mwaka 2024

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi