Ingwe wasaini mkataba wa miaka mitatu na Betika wa kima cha shilingi milioni 195

Klabu ya AFC Leopards imesaini mkataba wa  miaka mitatu wa kima cha shilingi milioni 195  na kampuni ya mchezo wa kamari ya  Betika .

Kulingana na  Betika mkataba huo utawezesha  kampuni hiyo kuwa mfadhili wa jezi za klabu hiyo ,  huku Leopards wakipokea shilingi milioni 65 kwa kila mwaka .

Mkataba huo utaanza kutekelezwa Agosti Mosi mwaka huu   ,kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu wa mwaka 2022 na 2023 ikiwa afueni kubwa  kwa Ingwe  ,ambao mkataba wa awali wa shilingi milioni 60  na kampuni ya Sportika ulisitishwa  mapema wiki hii.

Also Read
Omanyala ajiunga na National Police Service

Betika pia watakuwa wafadhili wa klabu ya Police FC inayoshiriki ligi kuu ya FKF .

Mwenyekiti wa Leopards Dan Shikanda amesema kuwa ufadhili huo utafaa pakubwa katika jamii ya Ingwei ,na kuondoa mzigo wa kulipia gharama za timu.

Also Read
Leopards yakwea hadi nafasi ya pili huku mashemeji Gor wakiinuka hadi nambari 5 ligini

“Tumekuwa tukiomba kupata mdhamini ambaye atatusaidia kuafikia malengo yetu ya kushinda taji ya ligi kuu na natumai kuwa sasa hatutakuwa na changamoto nyingi za kifedha ambazo zimekuwa zikitukabili,karibu sana Betika katika jamii ya Ingwe “akasema Shikanda

Kulingana na Brand Manager wa Betika Eric Mwiti ,wamejitolea kuendelea kuinua viwango vya kandanda nchini.

Also Read
Fulham yaenguliwa ligi kuu EPL kufuatia kipigo cha Burnley

“Katika ufadhili huu tunataka kuinua viwanago vya timu  na pia mashabiki  na ni hakikisho la  kampuni ya Betika  kuendelea kukuza soka ya humu nchini “akasema Mwiti

Ufadhili huo utazinduliwa baadae, kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa ligi kuu ya Kenya.

Betika imekuwa mdhamini mkuu wa Sofapaka kwa misimu miwili iliyopita .

  

Latest posts

Watu watatu wafariki kutokana na Covid-19 hapa nchini

Tom Mathinji

Rais Ruto: Serikali kudhibiti vilivyo makali ya njaa hapa nchini

Tom Mathinji

Mabingwa wa dunia Ufaransa na Uingereza waangukia pua katika droo ya kufuzu kwa kombe la Euro mwaka 2024

Dismas Otuke

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi