Ingwe watabasamu baada ya kuondolewa vikwazo vya usajili wachezaji na FIFA

Miamba wa soka nchini Kenya,AFC Leopards wameondolewa vikwazo na shirikisho la kandanda duniani FIFA kusajili wachezaji ,baada ya rufaa yao kufaulu dhidi ya difenda wa zamani Soter Kayumba aliyeishtaki timu hiyo kwa FIFA kwa kutomlipa .

Also Read
Wachezaji soka wa kigeni katika ligi za Ukraine na Russia waruhusiwa kuhamia vilabu vingine

Leopards wameshinda kesi hiyo baada ya Mnyarwanda huyo kushindwa kujibu rufaa hiyo kwa wakati ufaao iliyowasilishwa kwa FIFA .

Also Read
Engin Firat kuiga Harambee Stars Jumatatu baada ya mechi ya Rwanda

Ingwe walifungiwa ksuajili wachezaji katika wakati wa dirisha fupi la usajili msimu huu baada ya Kayumba kuwashtaki kwa FIFA.

Timu hiyo ilikuwa imeafikiana na mchezaji huyo kutatua kesi nje ya mahakama ,lakini Leopards wakalazimika kwenda kwenye mahakama ya FIFA ya kutatua rufaa za michezono kufuatia hatua ya beki huyo kukiuka makubaliano hayo.

  

Latest posts

Kalonzo: baadhi ya walioteuliwa kuwa Mawaziri si waadilifu

Tom Mathinji

George Kinoti amkabidhi mamlaka kaimu mkurugenzi wa DCI Hamisi Massa

Tom Mathinji

Rais Ruto abuni kamati ya kutathmini mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi