Ingwe yapigwa na stima huku Tusker wakikatwa makali na Mathare

Klabu ya Western Stima imewabwaga AFC Leoapards   mabao 3-2 katika mojawapo ya mechi tatu za ligi kuu  FKF raundi ya 27 ,zilizochezwa siku ya Jumanne katika uwanja ASK Nakuru .

Michael Karamor aliwaweka Stima uongozini kwa bao la dakika ya 13 kufuatia mkanganyiko wa mabeki wa Ingwe ,kabla ya kuongeza la pili dakika mbili baadae kupitia kwa penati  baada ya beki wa Chui  Rovert Mudenyu kushika mpira.

Also Read
Mamelodi na Belouizdad kuchuana Benjamin Mkapa jijini Dare salaam

Collins Shivachi alikomboa goli moja kwa Ingwe dakika ya 87 ,lakini Geofrey Ojunga akaongeza bao la tatu kwa Stima muda mfupi baadae ,kisha Bonface Mukhekhe akapiga bao la pili kwa Leopards dakika za mwisho na mech kumalizika kwa ushindi wa  Stima wa 3-2 .

Also Read
Gor Mahia walikuwa 'Bize' Sokoni huku dirisha la uhamisho wachezaji likifungwa
Also Read
Kenya yanakili visa 1,259 vipya vya Covid-19

Katika mapambano mengine Bandari Fc imetoka nyuma mara mbili na kulazimisha sare ya 2-2 na wenyeji Bidco United huku vinara wa ligi Tusker FC wakilazimishwa kutoka sare kapa dhidi ya Mathare united.

  

Latest posts

Police Fc washerehekea kurejea ligi kuu baada ya mwongo mmoja kwa dhifa

Dismas Otuke

Mwanafunzi ateketeza bweni kukwepa kufanya mitihani Tharaka Nithi

Tom Mathinji

Mahakama yamzuia Mohammed Badi kuhudhuria mikutano ya Baraza la Mawaziri

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi