Iran yamnyonga Navid Afkari licha ya shinikizo za kimataifa za kutotekeleza adhabu hiyo

Iran imemnyonga mwana mieleka mmoja aliyepatikana na hatia ya mauaji baada ya kuupuza wito wa jamii ya kimataifa wa kutotekeleza adhabu hiyo ya kifo dhidi yake.

Navid Afkari, mwenye umri wa miaka 27, alihukumiwa kifo baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mlinzi mmoja wakati wa wimbi la maandamano dhidi ya serikali mwaka wa 2018.

Shirika la habari la Iran lilipeperusha moja kwa moja kukiri kwa Navid kutekeleza mauji hayo.

Also Read
Mamia ya wanafunzi watoweka Nigeria baada ya shule yao kuvamiwa

Hata hivyo Navis alisema aliteswa ili kukiri mauaji ya mlinzi huyo kulingana na wakili na familia yake.

Wakili wake alisema hakukuwa na ushahidi kwamba Navid alitekeleza mauaji hayo.

Idara ya mahakama ya Iran ilipuuzilia mbali madai kwamba Navid aliteswa.

Navid Afkari na ndugu zake walikuwa wameajiriwa katika kampuni moja ya ujenzi eneo la Shiraz kilomita  680 kusini mwa jiji kuu Tehran.

Mahakama ya mkoa wa Shiraz pia iliwahukumu ndugu zake  Navid ambao ni Vahid Afkari na  Habib Afkari kifungo cha miaka  54 na 27  gerezani mtawalia.

Also Read
Ufaransa na Poland zarejesha masharti ya kudhibiti Covid-19

Wakili wa Afkari alilaumu utawala kwa kutokubalia familia ya mteja wake kumtembelea kabla ya kumnyonga jinsi inavyohitajika kisheria.

Chama kinachowakilisha wanariadha 85,000 duniani ni miongoni mwa wale waliotaka hukumu hiyo kusitishwa.

Shirika la michezo duniani kwa upande wake limesema Navid alilengwa na serikali ya taifa hilo maksudi kwa kuhusika kwenye maandamano hayo, na limetoa wito taifa hilo lisiruhisiwe kushiriki mashindano yeyote ya kimataifa.

Also Read
Mshauri wa Trump kuhusu Covid-19 Scott Atlas, ajiuzulu

Rais wa Marekani Donald Trump aliitaka Iran kumsamehe mwanamieleka huyo akisema kosa lake lilikuwa tu kushiriki kwenye maandamano dhidi ya serikali.

Kamati ya kimataifa ya olimpiki IOC imetaja kutekelezwa kwa hukumu hiyo ya kifo dhidi ya Navid kama tukio la kuhuzunisha na imeitakia familia yake faraja.

  

Latest posts

Babu wa Loliondo aliyepata umaarufu wa kutibu magonjwa sugu amefariki

Tom Mathinji

Israeli: Iran ilishambulia Meli ya kubeba mafuta katika Pwani ya Oman

Tom Mathinji

Australia kuwatumia wanajeshi kutekeleza masharti dhidi ya Covid-19

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi