Meja Jenerali N, anaingia katika kumbukumbu za kihistoria kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa katika wadhifa wa katibu wa kijeshi wa Rais wa Israeli Isaac Herzog.
Rais Herzog ameweka wazi kuwa ananuia kumteua mwanamke katika wadhifa huo, huku waziri wa ulinzi Benny Gantz na msimamizi wa wafanyikazi wa vikosi vya ulinzi vya Israeli Luteni Jenerali Aviv Kohavi, wakikubaliana na uteuzi huo.
N.mwenye umri wa miaka 40, ambaye ni mkazi wa Israel ya kati, atakuwa mwanamke wa kwanza kuhudumu katika wadhifa huo wa katibu wa kijeshi katika afisi ya Rais wa Israel. Atakapotwaa wadhifa huo, N atapandishwa cheo na kuwa Brigedia Jenerali.
āNā atachukua mahala pa Brigedia Jenerali Alaa Abu-Rukun, ambaye amehudumu katika wadhifa huo kwa muda wa miaka mitatu iliyopita.
N, ambaye ni afisa mkuu wa ujasusi, amehudumu katika vikosi vya ulinzi vya Israel kwa muda wa miaka 22, huku akishikilia nyadhifa mbali mbali.
Afisa huyo wa kijeshi,ameolewa na ana watoto wawili, na pia ana shahada katika historia ya mashariki ya kati.
Akimpongeza N., Herzog alisema atakaribishwa katika kundi la washauri wa Rais, huku taaluma yake ikiboresha afisi ya Rais, Vikosi vya ulinzi na kwa taifa la Israel.
Herzog alimshukuru Abu-Rukun kwa huduma yake katika Makao ya Rais na kwa mchango wake wa kupigiwa mfano katika vikosi vya ulinzi na taifa la Israel.