Israeli: Iran ilishambulia Meli ya kubeba mafuta katika Pwani ya Oman

Israeli inaishutumu Iran kwa kuhusika na shambulizi dhidi ya  meli ya  kubeba mafuta ambapo wafanyikazi wawili,  raia mmoja wa Uingereza  na mwingine wa Romania  waliuawa.

Meli hiyo  MV Mercer Street,  ambayo ni  ya kampuni   ya  Zodiac yenye makao yake   mjini   London, ilikuwa  kando ya  Pwani ya Oman kwenye  bahari ya  Arabia  kisa hicho kilipotokea mnamo  Alhamisi.

Also Read
Naibu Rais William Ruto asema hababaishwi na miungano ya kisiasa inayobuniwa

Kampuni hiyo ambayo inamilikwa na raia wa Israeli,  Eyal Ofer, ilisema kuwa  inachunguza kubaini kilichojiri.

Hata hivyo, waziri wa mashauri ya kigeni  wa Israeli, Yair Lapid alisema  kisa hicho ni  kitendo cha  kigaidi cha Iran.

Also Read
Boko Haram yadai kuwateka nyara wanafunzi kaskazini mwa Nigeria

Habari kamili  kuhusu meli hiyo iliyokuwa ikipeperusha  bendera  ya  Liberia  na ambayo  imesajiliwa  nchini Japan  hazijatolewa.

Kisa hicho kinaashiria kuongezeka kwa taharuki katika Kanda hiyo, huku baadhi ya ripoti zikiashiria kuwa ndege isiyoendeshwa na rubani ilihusika.

Also Read
Kutakuwa na maziwa ya bure siku ya kusherehekea kupandishwa hadhi kwa mji wa Nakuru

Msemaji mmoja wa serikali ya Uingereza, alisema nchi yake pia inajitahidi kubainisha ukweli kuhusu kisa hicho.

Na BBC

  

Latest posts

Daktari aliyewaua wanawe wawili kaunti ya Nakuru amefariki

Tom Mathinji

NCIC kuwatumia vijana kuwa mabalozi wa amani kabla ya msimu wa uchaguzi

Tom Mathinji

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuvuruga amani hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi