Israeli yaonya kuhusu ufaafu wa Rais Mteule wa Iran Ebrahim Raisi

Israel imesema jamii ya kimataifa inapaswa kuwa na wasi wasi kubwa kufuatia kuchaguliwa kwa Rais Mteule mpya wa Iran, Ebrahim Raisi.

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Israeli, Lior Haiat, amesema Raisi ndiye rais mwenye msimamo mkali zaidi wa Iran kuwahi kuchaguliwa.

Also Read
Trump aonywa dhidi ya kutumbukia mtegoni kuhusu madai ya vita kati ya Marekani na Israeli

Pia alionya kuwa kiongozi huyo mpya ataongeza shughuli za nuklia za Iran.

Ebrahim Raisi alitangazwa mshindi wa uchaguzi wa urais wa Iran hapo jana katika kinyang’anyiro ambacho kilionekana kuwa kilipangwa kumpendelea.

Raisi, ambaye ataapishwa mnamo mwezi wa Agosti, ndiye Jaji Mkuu wa Iran na anashikilia maoni ya kihafidhina.

Yuko chini ya vikwazo vya Marekani na amewahi kuhusishwa na kunyongwa kwa wafungwa wa kisiasa.

Also Read
Uchaguzi mkuu nchini Iran wavutia Idadi ndogo ya wapiga kura

Katika taarifa kufuatia ushindi wake, aliahidi kuimarisha imani ya umma kwa serikali, na kuwa kiongozi kwa taifa lote.

Also Read
Tetemeko la ardhi lasababisha vifo vya watu 20 Pakistan

Iran na Israeli zimekuwa katika hali ya uhasama kwa muda mrefu, hali ambayo imesababisha nchi zote mbili kushiriki katika vitendo vya kulipizana kisasi.

  

Latest posts

Tanzania kupokea dozi 500,000 aina ya Pfizer kufikia mwisho wa mwezi Oktoba

Tom Mathinji

Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai nchini Tanzania afungwa miaka 30 gerezani

Tom Mathinji

Mbunge Sir David Amess auawa kwa kudungwa kisu nchini Uingereza

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi