Issa Rae na Louis Diame wafunga ndoa

Muigizaji wa Marekani Issa Rae ambaye pia ni mwandishi na mtayarishi wa filamu amefunga ndoa na mchumba wake Louis Diame. Issa alitumia mitandao ya kijamii kutangaza kwamba walifanya arusi yao katika eneo la kusini mwa Ufaransa na ilihudhuriwa na jamaa na marafiki wa karibu.

Tangazo la Issa hata hivyo lilikuwa limejaa mafumbo tele wengi wangedhania ni picha tu. Chini ya picha za harusi aliandika maneno kama “Shughuli ya ghafla ya kupiga picha nikiwa nimeavaa nguo iliyoundwa na vera wang”, “marafiki zangu wa kike walikuja kunisaidia lakini ikawa sadifa kwamba walikuwa wamevaa nguo sawa”, “waliaibika sana” na “alafu nikasonga na mume wa mtu”.

Also Read
H_art The Band waitisha likizo.
Also Read
Gigy Money amlaumu Beyonce

Alishukuru kampuni ya kuandaa hafla za harusi ya white eden weddings kwa kuwaandalia tukio hilo na kulifanya kuwa la kipekee.

Mtaalamu wa mitindo ya mavazi Vera Wang ambaye alishonea Issa nguo yake ya harusi ndiye alidhibitishia umma kwamba kweli harusi ilifanyika kufuatia maneno ambayo aliandika chini ya picha hizo akimtakia Issa ndoa njema.

Also Read
Rotimi asherehekea mapenzi, siku yake ya kuzaliwa

Wageni waliohudhuria harusi walijumuisha waigizaji wenzake Yvonne Orji na Jay Ellis, ambao baadaye walichapisha picha zao wakiwa arusini.

Issa na Louis huwa wanaficha uhusiano wao na ulijulikana tu mwaka 2019 baada ya Issa Rae kupigwa picha na jarida la Essence akiwa amevaa pete ya uchumba.

  

Latest posts

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Harmonize Matatani Tena

Marion Bosire

Pday Hurrikane Azungumzia Uhusiano Wake na Nyota Ndogo

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi