Makala ya 33 ya kipute cha kuwania kokbe la Afrika Afcon yanatarajia kupata mabingwa wapya kwenye fainali ya Februari 6 ,kufuatia mabingwa watetezi kutemwa nje baada ya kipigool cha 1-3 na Ivory Coast.
Algeria pia wameandikisha historia kwa kufurushwa kwenye mashindano ya mwaka huu nchini Cameroon bila lushinda mechi wakizoa pointi 1 pekee .
Ivory Coast maarufu the Elephants wameongoza kundi E kwa pointi 7, moja zaidi ya Equatorial Guinea ambao pia wamefuzu kwa raundi ya 16 bora kufuatia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sierra Leone.