J. Cole Arejelea Mchezo wa Mpira wa Kikapu

Mwanamuziki wa mtindo wa rap Jermaine Lamarr Cole maarufu kama J. Cole amerejelea mpira wa kikapu kama mchezaji mwenye uzoefu katika safu ya ulinzi. Zamu hii atacheza nchini Canada na tangazo hilo lilitolewa na usimamizi wa ligi kuu ya mchezo huo nchini Canada kupitia Twitter. Tangazo hilo la Alhamisi lilisema kwamba mchezaji huyo wa umri wa miaka 37 amejiunga na timu ya “The Scarborough Shooting Stars” na atacheza kwa msimu mpya unaoanza Mei 25.

Also Read
IEBC kuongeza Idadi ya nchi za ugenini ambako wakenya watashiriki kwa upigaji kura

J. Cole wa umri wa miaka 37 na ambaye ana urefu wa futi sita na inchi tatu, alicheza mpira wa kikapu akiwa katika shule ya upili huko North Carolina nchini Marekani na akacheza pia kwenye ligi ya Afrika ya mpira wa kikapu mwaka 2021 chini ya timu ya Rwanda Patriots. Alitia saini mkataba wa kuchezea timu hiyo ya Rwanda mechi tatu pekee na akagura baada ya mechi hizo. Alizaliwa nchini Ujerumani lakini akalelewa Marekani.

Also Read
Obiri,Chepkoech,na Cheruiyot miongoni mwa mabingwa 12 watakapoambana Doha Diamond league Ijumaa

Cole alishinda tuzo ya Grammy mwaka 2020 kwenye kitengo cha wimbo bora wa mtindo wa Rap kupitia wimbo wake uitwao “A Lot” ambao alishirikishwa na 21 Savage. Ameshinda tuzo nyingi za BET na ana albamu sita ambazo zimemletea mapato mengi. Amewahi kushirikiana na wanamuziki tajika kama Kendrick Lamar, Janet Jackson na Young Thug. Albamu yake ya hivi karibuni zaidi inaitwa “The Off-Season” na ilitoka yapata mwaka mmoja uliopita.

  

Latest posts

Kenya Simbas yanusurika na kufuzu kwa fainali ya kombe la Afrika

DOtuke

Injera na Onyala kukosa nusu fainali ya Algeria baada ya kujeruhiwa

DOtuke

Harusi ya Nandy Kuwa ya Awamu Tatu

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi