Mahakama iko tayari kwa kesi za uchaguzi mkuu ujao asema Jaji mkuu Martha Koome

Jaji mkuu Martha  Koome amesema idara ya mahakama  iko tayari kusikiza na kuamua kesi zote zitakazotokana na uchaguzi wa mwaka ujao  ndani ya siku 90 kama njia moja ya kuhakikisha uchaguzi  huo utakuwa  huru na wa haki.

Jaji Koome ameyasema haya Jumanne katika taasisi ya Kenya School of government ,alipoongoza kikao  cha  maafisa wakuu serikali  kupanga mikakati ya uchaguzi mkuu wa mwaka ujao.

Also Read
Rais Kenyatta amuomboleza marehemu Badi Muhsin
Jaji mkuu Martha Koome akiwa na waziri wa usalama wa ndani Dr Fred Matiang’i

Hata hivyo Jaji Koome amefichua kuwa idara ya mahakama ina upungufu wa pesa kwenye bajeti yake ikiwa ni mapungufu ya shilingi milioni 710 katika bajeti ya matumizi ya pesa ya mwaka 2021 na 2022 na mapungufu ya shilingi bilioni 1 nukta 3 katika bajeti ya mwaka 2022 na 2023 ambayo inahitaji kurebishwa.

Also Read
Martha Koome aibuka mshindi kwenye kinyang’anyiro cha Jaji Mkuu wa Kenya

Jaji mkuu pia ameelezea haja ya bunge kufanyia marekebisho sheria za uchaguzi za mwaka 2017 ,  ili kushuluhisha baadhi ya changamoto ambazo idara ya mahakama ilikumbana nazo  wakati wa uchaguzi mkuu.

Mkutano huo ulihudhuriwa na waziri wa usalama wa kitaifa  Dkt Fred Matiang’i pamoja na katibu wake Karanja Kibicho,Waziri wa wizara ya Teknohama Joe Mucheru,Solicitor mkuu Ken Ogeto,mkuu wa sheria  Paul Kihara , Inspekta mkuu wa polisi Hillary Mutyambai  na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi na mipaka IEBC  Wafula Chebukati miongoni mwa viongozi wengine wakuu serikalini.

  

Latest posts

Rashid Aman: Chanjo zinazotolewa hapa nchini ni salama

Tom Mathinji

Kampuni ya sukari ya Nzoia yalaumiwa kwa kutowalipa wakulima

Tom Mathinji

China kupiga jeki uwezo wa kuzalisha chanjo hapa nchini

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi