Jamaa awadunga kisu watoto wake kwa kutilia shaka iwapo ndiye baba yao wa kweli

Watoto wawili wanauguza majeraha katika hospitali ya matibabu maalum ya Nyahururu, baada ya kudungwa kisu na baba yao katika mtaa wa Ziwani, Kaunti ya Nyandarua.

Inasemekana Ken Mburu aliwadunga kisu watoto hao wenye umri wa mwaka mmoja na miaka saba na kujaribu kuteketeza nyumba yao kabla ya kujidunga kisu.

Also Read
Serikali kuanzisha hazina ya kuwarejesha nchini wakenya wanaoteseka ughaibuni

Mshukiwa huyo anaendelea kupokea matibabu kwenye hospitali ambapo watoto wake wamelazwa.

Naibu chifu wa eneo hilo, Mary Kimani, alisema majirani walisikia watoto wakipiga mayowe, ndiposa wakafika hapo kuwanusuru.

Also Read
Mshukiwa wa msururu wa mauaji kaunti ya Nyandarua akamatwa

Majirani walisema mwanamume huyo amekuwa akizua rabsha akitaka watoto hao wafanyiwe uchunguzi wa DNA, ili kubainisha ikiwa yeye ndiye baba-mzazi wa watoto hao.

Maafisa wa polisi wa kituo cha Mairo Inya walimnusuru mwanamume huyo kutoka kwa wananchi waliotaka kumuua, kufuatia kisa hicho.

Also Read
Mwanafunzi akiri mashtaka ya kumshambulia mwalimu wake Nyandarua

Gari la wazima moto la kaunti ya Nyandarua lililokuwa likielekea mahali hapo kuzima moto huo, hata hivyo lilianguka kwenye barabara ya kutoka Nyahururu kuelekea Ol Kalou.

  

Latest posts

Wanjigi: Kenya haina uwezo kuwapa wasio na ajira shilingi 6,000 kila mwezi

Tom Mathinji

Mwanaume ajitia kitanzi baada ya kuteketeza nyumba yake eneo la Gichugu

Tom Mathinji

Viongozi wa kaunti ya Murang’a wampendekeza Peter Kenneth kwa wadhifa wa naibu rais

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi