Jamii zisizojiweza kunufaika na msaada wa bima ya afya kaunti ya Migori

Serikali ya kaunti ya Migori ikishirikiana na tawi la bara Afrika la shirika la afya  Amref, imezindua shughuli ya kiuchumi na kijamii ya kubaini jamii zisizojiweza zinazotarajiwa kunufaika na msaada wa bima ya afya.

Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za kuafikia mpango wa afya bora kwa wote almaarufu-UHC hapa nchini.

Also Read
Serikali yatangaza tarehe 10 Octoba kuwa siku kuu ya kitaifa

Habari zitakazokusanywa zitajumuishwa kwenye sajili ya serikali ya taifa ya kusaidia jamii na zitawezesha kubaini jinsi pesa hizo za msaada zinavyotumika.

Shughuli hiyo ambayo imefadhiliwa na wakfu wa Bill and Melinda Gates kupitia shirika la Amref, ni nguzo muhimu katika mpango wa upatikanaji wa afya bora kwa wote.

Akiongea na wanahabari, mkurugenzi wa shughuli za kibunifu wa shirika la Amref, Caroline Mbidyo alisema wahudumu wa afya wa kijamii watakusanya habari nyumba kwa nyumba kwa kutumia mfumo wa usimamizi wa habari za afya katika jamii CB-HMIS uliozinduliwa na kitengo cha ubunifu cha shirika la Amref.

Also Read
Wanawake wanaougua Fistula kunufaika na Matibabu bila malipo katika hospitali ya Kenyatta
Also Read
Kenya yanakili visa 98 vya maambukizi ya COVID-19

Alisema habari hizo zitakazokusanywa zitajumuishwa kwenye sajili ya serikali ya taifa ya kusaidia jamii na zitawezesha kubaini jinsi pesa hizo za msaada zinavyotumika.  

  

Latest posts

Familia ya Mbijiwe yatoa wito kwa Rais Ruto kusaidia kumpata mwana wao

Tom Mathinji

Uchukuzi kutatizwa katika barabara ya Lang’ata mwishoni mwa Wiki

Tom Mathinji

Kaunti za Isiolo na Siaya zamulikwa kwa ufujaji wa fedha

Tom Mathinji

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi