Jay Z azungumzia familia

Mwanamuziki wa Marekani Jay Z ni mume wa mwanamuziki mwenza Beyonce na pamoja wana watoto wanne ambao ni Blue Ivy, Nine na mapacha Rumi na Sir.

Tofauti na watu wengine maarufu ulimwenguni wawili hao hawapendi kuzungumzia ndoa yao na familia yao kwenye mahojiano lakini Jay Z alifunguka kiasi alipohojiwa maajuzi na jarida moja la Uingereza.

Jay Z ambaye jina lake halisi ni Shawn Corey Carter anasema kwamba anaelewa msukumo ambao watoto wao huenda wakahisi kutokana na umaarufu wa wazazi wao lakini wanawaunga mkono kwa kila watakacho kukifanya maishani.

Also Read
Jaji Mkuu Martha Koome awahimiza majaji kutekeleza majukumu bila hofu

Kulingana naye, hawatumii mtindo wa malezi ambapo mzazi anachagulia mwanawe njia ya kufuata maishani kwa nia labda ya kupata mrithi atakayeendeleza biashara na taaluma yake.

Badala yake, alisema yeye na mke wake Beyonce wametengenezea watoto wao mazingira ya kuhisi upendo na uungwaji mkono kila mara.

Mwanao wa kwanza Blue Ivy anaonekana kuchagua kufuata nyayo za mamake katika muziki kwani amewahi kuhusishwa kwenye wimbo ambao ulishinda tuzo la Grammy. Blue Ivy husaidia mamake pia katika biashara yake ya mavazi ambapo huwa anaonekana kwenye picha za mauzo ya mavazi hayo.

Also Read
Anne Kansiime atangaza kwamba anatarajia mtoto

Jina lake “Ivy” limetumika pia katika jina la mitindo hiyo ya mavazi ambayo inaitwa “Ivy Park”.

Wengi hutizama ndoa ya wanamuziki hawa wawili ambao pia ni wafanyibiashara kama ambayo imekamilika na haina shida kama ndoa nyingine ulimwenguni lakini sivyo.

Mwaka 2018, Jay Z kwenye mahojiano alisema kwamba ilibidi aelewe jinsi sha kushughulikia hisia zake kupitia njia kama vile kuzizungumzia na mpenzi wake na hivyo akaokoa ndoa yao ambayo ilikumbwa na matatizo wakati fulani.

Also Read
Beyonce ajiunga na miito ya mabadiliko ya polisi nchini Nigeria

Hakutaja tatizo hilo.

Kuhusu mabadiliko yaliyoletwa na janga la Corona, Jay Z alielezea kwamba sharti la kukaa nyumbani lilipoanza kutekelezwa, walitumia wakati huo kama familia kukaa pamoja.

Kadri muda ulivyosonga walijifunza jinsi ya kuishi na janga la sasa la virusi vya Corona.

Jay Z na Beyonce walifunga ndoa mwaka 2008 huko Ney York tukio ambalo halikuangaziwa sana na umma kulingana na mapenzi yao.

  

Latest posts

Kenya yapokea dozi 795,600 aina ya Pfizer kutoka Marekani

Tom Mathinji

Nelson Havi awasilisha rufaa ya kusimamisha mtaala wa CBC

Tom Mathinji

Adasa Afichua Sababu ya Kimya Chake

Marion Bosire

Tovuti hii inatumia kuki kukuhudumia vyema. Tafadhali kubali kupokea. Kubali Fahamu Zaidi