Kiongozi mpya wa jeshi nchini Burkina Faso ameahidi kurejesha utawala wa kikatiba.
Kiongozi huyo Lutena kanali Paul-Henri Damiba aliongoza kundi lililomwondoa mamlakani rais Roch Kaboré siku ya jumatatu.
Alimlaumu rais huyo kwa kushindwa kukomesha mapigano ya wanamgambo wa kiislamu.
Akiwa amevalia sare za kijeshi, luteni kanali Damiba jana alihutubia taifa hilo kwa mara ya kwanza kupitia runinga ya kitaifa tangu alipoingia madarakani.
Kiongozi huyo mwenye mri wa miaka 41, alisema atakutana na wawakilishi wa sekta ngazi mbali mbali katika jamii kujadili namna ya kufanya mabadiliko.
Aliongeza kwamba Burkina Faso inahitaji washirika wa kimataifa sasa kuliko awali kufuatia shutma dhidi ya mapinduzi hayo.
Burkina Faso ni taifa la tatu la Afrika magharibi kushuhudia mapinduzi ya kijeshi katika siku za hivi punde.
Guinea na Mali zimewekewa vikwazo na shirika la kiuchumi la mataifa ya Afrika magharibi-Ecowas ili kuzishinikiza kurejelea utawala wa kikatiba baada yua mapinduzi.
Shirika la Ecowas litakutana siku ya Ijumaa kujadili jinsi ya kushughulikia mapunduzi hayo ya hivi punde katika eneo hilo.